Kwanza ni Wimbo siyo nyimbo pia naona hauujui muziki kama ulivyoandika.
Aslay nyimbo zote anaimba kwa melody ile ile na mixing ni ile ile ndani ya miezi miwili ametoa nyimbo zaidi ya 14 huyu siyo msanii wa kawaida, hao wanaomsikiliza hawajui muziki kama wewe tu.
Ninavyojua Shilole kaimba na Iyo remix ya Kiki, ule wimbo siyo sawa na za kipindi kile anashindana na Snura ambaye kwa sasa ni utumbo mtupu. Hatua ya sasa ya Shilole yule mpinzani wake haiingii.
Wimbo wake mpya najua unaitwa Kigoli sijui huo unaousema wewe ni upi.
Joh Makini na Davido na Madee na Tekno wamezingua, kwa kua Joh anaendekeza mistari ya kitoto sawasawa na mdogo wake Niki wa 2. Kati ya Madee na Joh ni bora wimbo wa Joh utausikiliza na usingizi utakuja.
Madee na Tekno nakubaliana na wewe ni utumbo kuanzia Tekno mpaka Madee mwenyewe, Cabo Snoop katoa ngoma inaitwa Awaa huyu ni jamaa alikuja kufanya show Tanzania na mkalimani lakini kwenye huu wimbo kaimba Kiingereza, ameamua kubadilika na kufuata soko. Wasanii wetu bado wamelala.
Washauri wa wasanii wana mapengo kwenye ubongo.