Wasanii wa Bongo fleva na Bongo movie wavutiwa na biashara ya makanisa

Anthony10

Member
Sep 13, 2016
91
102
Watu waliofungua/kumiliki Makanisa Binafsi wamejikuta wakipata utajiri ambao hawakuufukiria hivyo BIASHARA hiyo imewavutia watu wenge hasa watu maarufu

Nay wa Mitego anasema anafungua kanisa lake la kumuabudu Mungu aliye hai. Rapper huyo amejinadi kuwa anatarajia kupata waumini wengi kupitia kanisa lake na kwamba litakuwa chanzo cha mafanikio katika mambo yao.

"Ninawaheshimu watumishi wa Mungu wote duniani, ila sifungamani na wachungaji (Pastors) wanaofanya dini bishara. siku hizi wanafanya mpaka promotion makanisa yao, MUNGU WANGU ATA DEAL NA NYINYI ROUND HII" - Nay wa Mitego.

VITA NZITO! Baada ya Nay wa Mitego kutangaza nia ya kuanzisha kanisa lake Mchungaji Lusekelo aka Mzee wa Upako amtabiria mabaya ."Nay ni mtoto mdogo sana,hana akili ,kama ana wazazi wamuonye ,anakufulu nampa mika mitatu Tu atatembelea kuacha,Mungu hazihakiwi"

UWOYA kuwa mchungaji, atangaza kuanzisha kanisa
WEDNESDAY , 22ND FEB , 2017
Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema kuwa ana mpango wa kuwa Mchungaji pamoja na kumiliki kanisa lake yeye mwenyewe siku za usoni na kwamba anamuomba Mungu kila siku aweze kutimiza ndoto hizo.

"Nina ndoto ya kuwa mchungaji na kila siku huwa nina muomba Mungu anifanikishie suala hilo niweze kutimiza japokuwa sasa hivi bado nipo katika changamoto kubwa ila natumai ndoto zangu zitatimia. Natamani kuwa pastor ambaye ni mwalimu, niwafundishe watu Mungu anataka nini, lakini sitaki kuanzisha kanisa kama biashara, sitaki kucheza na Mungu, ndiyo maana najipanga kwanza sitaki kukurupuka, nataka niwafundishe watu Mungu anataka nini, na jinsi ya kumuomba Mungu"

BIBLIA IMEANDIKA
Mhubiri 12 : 13 - Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

Kushika amri za Mungu[10] na SABATO YAKE [amri ya NNE] ndio wajibu WA KILA anayeitwa MTU.

Njia hii inahitaji KUJitahidi kuiingia, huu ni mlango ulio mwembamba, kwa maana Yesu anasema kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze..usichelewe/usikawie/inuka ukatii sabato ya BWANA Mungu wako ,ukatii amri zake
Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.Luka 13 : 24 1 Yohana 5 : 3 -

NINI MAONI YAKO?
 
Back
Top Bottom