Wasakiziaji "Bill huko Bar" kwa Wenzenu Endeleeni kunichukia tu

Chawa wa Zamani

Senior Member
Mar 12, 2023
113
154
Naomba niwasalimie kihindi (kule walipo Mawazir 9 ) Kemcho ! kemcho!

Ni hv mtu unampigia Simu rafiki yako aje sehemu unayokula Bata wew..tena pengne kwa kumplease kabisaaa.. kwamba bila wew Mwamba hakuna vibe..

Basi kwa Hekima za kiurafk (na ulikuwa huna ratiba hio ) ukizingatia ni usiku pengne mpk Saa 7 nk.. unasema ngoja nikanywe bia hata mbili ili mwana apate company nk..

Hamadi!! unafika pale jamaa anakuchangamkia kweli huku akisema Haya si ndo mambo ...wew ukifurah mara waiter huyo kakupa mbili tatu...huku wao tayr washakimbiza balaa la heineken,jurgemaster,Hennesy nk...

Cha kushangaza ! inakuja Bill unaaambiwa na wew uchangie ...khaa!!!...umesikiaa wapi!!!! huku wakijinasibu asubuh watanilipa weeh! naijua hio!!

kufupisha story nlkuwa natoa elfu 20 tu..ili nisionekane nimekuja bila hela kisha najifanya naelekea Choon huku nikjua bolt ananisubr nje kisha natokomea kama mdudu ''FUKUFUKU' ama 'PANZI'

Lakini kwasasa siendi kwa hivyo vikao vya hao Watu wenye Calibre hio na nikimjua huwa namcancel kinyamwezi stori poa ila kweny bia zake kisha baadae nasakiziwa Bill hapana!! nawajibugi tu nipo mbali sana!

Mie binafsi nikimwita mshkaji kula Bata nahakikisha kila kitu nanunua mimi labda atoe kwa kupenda lkn sio kumsakizia alipe hapana bana ,hata zile bar zangu pendwa mfano 1245,the uncles na Gentleman Sinza nikiendaga mwenyew nakunywa mwenyew nasepa zangu fasta hata kuwe na Demu mithiri ya Nancy sumari simnunulii aendelee kule vishort vyao na Ndimu ...

Nyie jamaa wa hvy Mnajidharirisha kweli acheni hio tabia ya kimasikini wapuuzi nyie hata kama mkichukia lkn ndio hvyo ..na Sasa ni Rasmi Endeleeni kunichukia kwa ujuha wenu wa kimasikini na kishamba!
 
na watauona na ninajua kabisa humu wako kwena baadhi huwa n wadau wa huu mtandao pendwa !! tabia yao n mbovu sana!
 
Back
Top Bottom