Waraka wangu kwa Sekretariat ya ajira

raisi2020

Member
Mar 4, 2016
82
83
Habarini wandugu wote,katika historia ya maisha tumesoma binadamu alikuwa na maisha ya kuhamahama katika hali ya kujitafutia maendeleo,tulikuwa katika zama za mawe tukaja zama za chuma,sasa tupo kwenye Teknolojia kubwa kubwa sana hii yote ni kutokana na mahitaji ya kimaisha ya kila siku ya mwanadamu.Mpaka tumefika hapa yote ilikuwa ni jitihada za mababu na mabibi katika kuhamahama kwao na kutupelekea na sisi leo tujivunia tupo tunaishi.

Nije kwenye mada kuu,Nimeshuhudia maombi mengi hasa ya Secretariat ya Ajira TZ ikitoa maombi kwa kulazimisha watu ambao wapo katika utumishi wapitishe maombi yao kwa waajiri wao,ni sawa sijakataa inaweza ikawa na maana kubwa mno,ila sidhani kama wanafahamu roho mbaya tulizonazo sisi waafrika katika kuchukia maendeleo ya mtu mmoja mmoja,sidhani kama wanafahamu ubinafsi tulionao sisi waafrika hususani katika maisha yetu binafsi na familia zetu.

Watu walio katika utumishi wengi wao wanapata changamoto kubwa mno katika zoezi hili la kupitisha maombi hayo kupitia kwa waajiri wao,wengi wanaandikiwa majibu yasiyo lidhisha kwa kuwakwamisha tu kwa kuandika comments za hovyo hovyo,ndio mana nilianza na historia fupi ya mwanadamu,huyu mfanyakazi anapopata wazo la kuandika maombi sehemu ina maana yupo katika harakati za kujikwamua na kitu flani katika maisha yake.Huwezi kumzuia kwa ubinafsi wako na Taasisi yako.

Sasa je mnafanyia kazi vipi barua za watu kama hawa,na kama mnazitupa mbali hamtakuwa mnafanya fair katika kumsaidia huyu mtu mana nilitanguliza maneno ya ubinafsi,choyo,maugomvi haya yote yanaweza kusababisha muajili kukwamisha maombi ya mfanyakazi.

Rai kwa serikali yangu,naomba watu kama hawa waitwe kwenye interview kama watabahatika kupata nyinyi ndio muwe msaada kwa mtu huyu mana wengi wanakufa na matatizo yao katika Taasisi hizi hususani Taasisi kama za vyuo vikuu vyenu wanataabia kama hizi sana.
 
Majitu kama haya ndio yanabania juniors kupata kazi ridhikeni na mlipo maendeleo siyo mshahara Bali mipango.... Maisha lini kuhama hama mkifata mishahara mikubwa..... Endeleeni kupewa ripoti mbaya hivyo hivo
 
Majitu kama haya ndio yanabania juniors kupata kazi ridhikeni na mlipo maendeleo siyo mshahara Bali mipango.... Maisha lini kuhama hama mkifata mishahara mikubwa..... Endeleeni kupewa ripoti mbaya hivyo hivo
miafrika ndivyo tulivyo,jobless ila una roho mbaya ukija kuwa bosi je?
 
Back
Top Bottom