Waraka wa wazi kwa Mkurugenzi wa Geita mjini

mwananyaso

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
2,843
3,128
Habari mkurugenzi,

Ni matumaini yangu umzima wa afya ukiendelea kuchapa kazi barabara ili kuwaletea wana Geita mjini maendeleo.

Ndugu mkurugenzi husika, kama ada,linapotokea jambo ambalo sisi wananchi wa eneo husika tukiona jambo haliko sawa basi kupitia jukwaa hili hupenda wewe ulifahamu na kama kuna hatua za haraka uweze kuzichukua kwa manufaa ya wana Geita mjini.

Hii ni mara ya pili nakuandikia kuhusiana na kero za barabara za mitaa, baadhi ya mitaa hasa kata ya kalangalala mtaa wa Mbugani zina hali mbaya sana.

Ifahamike watabiri wametabiri kutakuwa na mnvua nyingi sana, ikihisiwa ni elinino ,hii italeta usumbufu sana kwa wakzi wa eneo husika bila hatua madhubuti kuchukuliwa,natambua kuna hatua zinafanyika site ,

Nimefuatilia kujua ni kiasi gani cha pesa ulichotenga kuhusu miundombinu ya barabara wewe na jopo lako la madiwani.

Mfano: Kata ya Kalangalala imetengewa (milioni tisa) na ina jumla ya mitaa kumi na moja, hii kata ni kubwa sana na kuna taarifa inatakiwa kugawanywa zitoke kata mbili,

Ndugu mkurugenzi hii kwa kweli si sawa,ukilinganisha na vyanzo vya mapato vilivyopo, kata hii ni ya mjini, na ndio reception ya mkoa.

Ukigawanya hiyo milioni tisa kwa mitaa kumi na moja almost kila mtaa unapewa laki Saba,mtaa wenye wakazi elfu sita unapokea laki saba za barabara are we seriously madame director?

Kuna mambo sisi wananchi tumeyabaini na huu ni ushauri wetu kwako

1: Inahitajika kusafishwa mtaro wa maji jirani na karavati la msuka posho mill upande wa kulia kama unakwenda nyankumbu, angalau mita mia tatu ili maji yanayotoka mjini yapate kwenda kasi kuelekea bwawa lililoko lake view hotel, bila hivyo hayo maji yatasambaa kwenye makazi ya watu inaweza sababisha uhalibifu wa mali na kugharimu maisha ya watu."Prevention is better than cure"

Upande tajwa ni kama umeziba,tuma wataalumu wako wakague, ili upanuliwe kuruhsu maji kukimbia haraka

2: Tunakuomba mkurugenzi wetu, wewe na madiwani wako hebu itisheni kikao cha dharura ,jalibuni kufikiria upya namna kuongeza pesa.za miundombinu hasa barabara za mitaa na caravat zake

3: Ni kuhusu hiyo grader yako ya halimashuri ,haina nguvu kabisa ya kukwangua kuna maeneo inaparaza tu badala ya kukata , kwakua fungu lipo kwanini msiongeze mashine hata moja ya kukodi zifanye kazi haraka kukimbiza muda kabla ya mnvua za vuli hazijashamiri?

4: Operotar wa gredar awe anapimwa pombe randomly ,ataiua hiyo mashine mspokuwa makini
 
Ukifika viunga vya Geita na sifa nilizozisikia ni vitu viwili tofauti,yaani mbingu na ardhi,wanakamua dhahabu ile mbaya, miundombinu ni ya kiporipori kweli kama kijiini tu hasa kando ya centre mji
 
Pesa tumepata asilimia 10 tu ya pesa ya matengenezo ya barabara za wilaya.

Sasa kwa pesa hiyo kiduchu, tutengeneze barabara ipi na tuache ipi?

Ndiyo maana tumeona ni bora tuitumie hiyo pesa tuitishe vikao vya ndani kujadili mbinu na mikakati endelevu ya kurekebisha hizo barabara.

Kama sehemu unayokaa sasa barabara zake ni mbovu, basi nakushauri uhamie sehemu nyingine; maana hatutengenezi barabara hizo leo wala kesho.
 
Pesa tumepata asilimia 10 tu ya pesa ya matengenezo ya barabara za wilaya. Sasa kwa pesa hiyo kiduchu, tutengeneze barabara ipi na tuache ipi? Ndiyo maana tumeona ni bora tuitumie hiyo pesa tuitishe vikao vya ndani kujadili mbinu na mikakati endelevu ya kurekebisha hizo barabara.
Kama sehemu unayokaa sasa barabara zake ni mbovu, basi nakushauri uhamie sehemu nyingine; maana hatutengenezi barabara hizo leo wala kesho.
Majibu ya mpumbavu,achieni ngazi mmeshindwa kazi, waingie viongozi wenye maarifa na uchungu na wakazi wa Geita,sio hii bla bla ya miaka nenda rudi

Kuwa kwenye ODC si kigezo cha ubora,nyie ndio wale mnaonunua nafasi za uongozi,na haya ndio huwa majibu yenu,
 
Halmashauri ya geita inataka kuwa kama Kilimanjaro(Moshi).
Majungu kila sehemu...mwambieni msukuma wa nzera amsemeee kwa rais
 
Pesa tumepata asilimia 10 tu ya pesa ya matengenezo ya barabara za wilaya. Sasa kwa pesa hiyo kiduchu, tutengeneze barabara ipi na tuache ipi? Ndiyo maana tumeona ni bora tuitumie hiyo pesa tuitishe vikao vya ndani kujadili mbinu na mikakati endelevu ya kurekebisha hizo barabara.
Kama sehemu unayokaa sasa barabara zake ni mbovu, basi nakushauri uhamie sehemu nyingine; maana hatutengenezi barabara hizo leo wala kesho.
Hiyo mashine imepaki hapo Mashapale siku ya pili leo badala ya kuwa site,kwa maana jana siku nzima na leo pia nini tatizo?,
Baadae muijazie Hours pesa mle?,safarii hii patachimbika tumejipanga
 
Back
Top Bottom