Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 726
- 953
Bismilahir Rahmanir Rahiim
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
S.L.P. 2055 DAR ES SALAAM.
WARAKA WA IDD - Shawal 01, 1445 - April 10, 2024
Awali ya yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kutupa fadhila nyingi. Tunamuomba azidi kuturehemu kwa hili na mengine.
Waandaaji wa mkutano huu, kwa furaha kubwa tunawapongeza waliofunga swaumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kutekeleza amri hiyo kubwa kutoka kwa Mola Muumba. Kuacha kula na kunywa unavyovipenda si jambo dogo. Kuacha unacho kitamani kwa mwenza wako ni jambo la subira kubwa na utiifu kwa Mola Muumba. Tunawatakia mafanikio wafungaji (na wasiofunga kwa nyudhuru mbalimbali za kisheria), na tunamuomba Mwenyezi Mungu apokee ibada hiyo tukufu waliyoitekeleza.
MAFUNZO YA RAMADHANI
Ubinadamu
Ramadhani ni ibada katika Uislamu. Aidha kijamii hubeba misingi ya mafunzo muhimu. Utafiti unathibitisha ina mafundisho mengi yanayo hitajika katika ustawi wa jamii. Utekelezaji wa nguzo hii, mtu hukaa na njaa na kiu ya maji kwa saa 12. Hufanya hivyo kwa siku 29, mpaka 30. Wataalamu wa maumbile ya binadamu wanasema seli za mtu aliyefunga hubeba hisia za njaa na kiu kwa kiasi kikubwa.
Mtu aliyeathirika na mafunzo ya Ramadhani, huwa na huruma kwa watu hasa wa tabaka la chini ambao kipato chao ni duni. Mtu huyo anapopata taarifa ya uhaba au ukosefu wa chakula au maji kwa mtu au kitongoji au taifa hupata hisia za janga hilo na hushughulikia kwa dhati tatizo hilo.
Jambo lingine katika Ramadhani ni Ucha Mungu. Uchaji Mungu ni tabia pana inayotufundisha nidhamu na utii bila ya kulazimishwa. Aliyefunga hutii amri ya kuacha kutumia milki yake ya halali. Huacha kusema uongo, kudhulumu, hutenda wema kwa viumbe na hutumia vizuri muda na rasilimali nyingine.
Matendo hayo kwa upana wake hubadili tabia ya mtu na kupelekea kupata hadhi inayopendwa na watu wengi “Ucha Mungu”. Kwa ufupi semina ya Ramadhani humtengeneza “Mtu wa Watu”.
Uadilifu
“Mtu wa Watu” anao wajibu mkubwa wa kijamii. Anawajibika kutafakari na kuchukua hatua muhimu kutengeneza jamii. Moja ya nguzo kubwa za ustawi wa jamii ni Uadilifu. Uadilifu ndio uti wa mgongo wa ubinadamu na maendeleo. Kukosekana kwa hilo ndio janga kuu katika mataifa yetu.
Katika ukomavu wa tatizo hilo, hivi karibuni watawala Tanzania wamepitisha sheria iliyowawezesha kuwaingiza familia zao (wake zao), katika mishahara mikubwa inayolipwa na serikali bila ya wao kuajiriwa. Watalipwa mamilioni hayo sambamba na kulipiwa gharama za matibabu ndani na nje ya nchi mpaka Tanzania itakapofutika katika ramani ya dunia.
Wakati wakipitisha sheria hiyo ya mgao wa fedha za umma kwa familia zao, raia, wagonjwa maskini wanalazimishwa kulipa shilingi 200,000, kila siku katika hospitali za serikali ili wapatiwe matibabu ya kusafisha figo zao. Wagonjwa hao wa figo husafishwa mara mbili au mara tatu kwa juma, hivyo hutozwa shilingi 600,000, kila juma katika hospitali hizo za serikali.
Kwa kuwa wengi wao ni watu maskini hushindwa gharama hizo na hufariki majumbani mwao. Wale wanaopata kianzio (kinachowawezesha kupokelewa hospitali), wanapofariki maiti zao huzuiliwa mpaka jamaa zao walipe gharama za matibabu ya maiti huyo.
Kama tulivyosema huko nyuma matarajio kwa wale walioshiriki Ramadhani wakastafidi mafunzo yake, watayaingiza katika jamii zetu. Mafundisho hayo yatumike kujenga uongozi bora wa familia na taifa kwa ujumla. Dhamana ya uongozi wapewe wale wenye utu na huruma kwa binadamu wenzi wao. Wapewe Waadilifu na Katu wasipewe watu wasio na hisia za utu kwa wengine.
Sheria
Jambo lingine la wajibu wa “Mtu wa Wau” ni suala la sheria. Hili ni jambo muhimu katika ustawi wa jamii. Hapa kwetu Tanzania hilo ni janga kwa raia wa tabaka la chini. Mtu hukamatwa na vyombo vya dola (mathalan) kwa tuhuma ya mauaji. Dola humpeleka mtu huyo mbele ya mahakama na kutamka kuwa inamshitaki kwa kufanya mauwaji. Halafu mkamataji (dola) huiambia Mahakama kuwa hawana ushahidi wa shauri hilo, hivyo Mahakama imnyime mtu huyo dhamana awekwe gerezani mpaka wao watakapopata ushahidi. Mahakama ya Tanzania hukubali maombi hayo na mtu huyo hukaa gerezani kati ya siku moja mpaka miaka kumi au zaidi.
Hapa chini tunaweka jedwali la baadhi ya Masheikh waliokamatwa na dola toka mwaka 2013 mpaka 2022, kwa madai ya kufanya ugaidi. Mpaka sasa Masheikh hao wanashikiliwa jela kwa miaka 2, 8, 9 na 11, kwa sababu hizo:
NA. JINA LA MAHABUSU NAMBA YA
KESI SHTAKA MIAKA GEREZANI
(Hawa ni wale waliosalia magerezani. Baadhi yao baada ya kuwekwa mahabusu kwa miaka mingi wamehukumiwa bila uthibitisho, vifungo vikubwa vya miaka 7, 10, 20, 30 na 50. Wengine 15, wamehukumiwa kunyongwa mpaka kufa). Sababu kubwa za raia hawa kunyimwa haki za msingi ni tatu:
1. Upande wa Serikali kushindwa kuendesha Mashauri kwa madai ya kutafuta ushahidi.
2. Upande wa Serikali kutoleta mashahidi Mahakamani kama sheria inavyowataka.
3. Kufutwa mara kwa mara tarehe zilizopangwa kusikilizwa mashauri hayo mpaka mwisho na kutokuwepo taarifa za lini mashauri hayo yataanza kusikilizwa tena.
Kama tulivyosema huko nyuma, matarajio kwa waliofunga “Mtu wa Watu” ni kuyaingiza mafundisho ya Ramadhani katika jamii. Mafundisho hayo yatumike kujenga uongozi bora. Dhamana ya uongozi wapewe wale wenye utu na huruma kwa binadamu wenzi wao. Na katu wasipewe watu wasio jali sheria na kutenda haki sawa kwa wote.
Usalama
Lingine katika kuangalia wajibu wa “Mtu wa Watu” ni suala la Usalama. Raia ndio ambao wanaunda serikali. Wajibu wao ni kulipa kodi ili kuijengea uwezo serikali. Wajibu wa serikali ni kuwalinda raia na mali zao. Tanzania raia wanalipa kodi lakini ulinzi wa serikali kwao haueleweki.
Mwaka 2023, Shura ya Maimamu Tanzania ilitoa taarifa ya uchunguzi. Katika kurasa za 48, 49, 50, 51 na 52 pia 53, 54, 55, 56, 57 na pia 58, 59, 60, 61, na 95, taarifa hiyo imeorodhesha majina 236, ya raia waliotekwa na kupotezwa kabisa ndani ya kipindi cha miaka kumi. (Inakisiwa taarifa hii ni ndogo sana ukilinganisha na manung’uniko ya raia waliopoteza watu wao. Nje ya ripoti hiyo raia wanaendelea kufikwa na janga hilo kama ambavyo hivi karibuni tarehe 7.3.2024, Sheikh Abdurazak Mohammed ametekwa huko Tunduru mkoani Ruvuma).
Katika taarifa hiyo yenye kurasa 129, kurasa 51, zimechapwa picha 135, za baadhi ya raia waliotekwa na kupotezwa. Miongoni mwao ni Masheikh Maimamu, Wanawake, Wanasiasa, Wafanyabiashara, Wakulima na Watoto wenye umri kati ya miaka 8 na 14.
Matukio ya raia kuuliwa na vyombo vya dola ni mengi mno Tanzania. Baadhi yao hutangazwa kuwa ni wezi, na vibaka. Lakini jambo la kushangaza tuhuma na operesheni hizo hufanywa kwa raia wa kawaida bila kuwagusa wakubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha wa Serikali (CAG), ya nyuma na ya mwaka huu 2022/2023, zimejaa taarifa za ufisadi mkubwa wa mabilioni ya fedha za umma uliofanywa na wakubwa waliokabidhiwa madaraka. Hata hivyo hakuna yoyote kati yao aliyechukuliwa hatua japo ya kufukuzwa kazi na kutakiwa arejeshe mali alizohodhi.
Raia wanao uliwa na vyombo hivyo vya dola hunyimwa haki hata ya utetezi ingawa Katiba ya nchi inaelekeza kufunguliwa mashtaka mahakamani mtu yoyote aliyemuuwa mwingine.
Kama tulivyosema huko nyuma, matarajio kwa wale waliofunga Ramadhani na kuathirika na mafundisho yake “Mtu wa Watu”, ni kuyaingiza mafundisho ya hayo katika jamii. Mafundisho hayo yatumike kujenga uongozi bora. Dhamana ya uongozi wapewe wale wenye utu na huruma kwa binadamu wenzao. Wenye uwezo wa kubeba jukumu la ulinzi kwa raia na mali zao.
Uongozi
Lingine ni suala Uongozi. Taifa ni mali ya raia wote, wakiwa na haki sawa katika rasilimali na uongozi. Itifaki ya uongozi ni kupokezana kisheria. Tanzania kuna tatizo kubwa katika mfumo wa sheria. Tatizo hilo limeleta ugumu kwa watanzania kupokezana uongozi wa taifa lao. Ugumu huo umekuwepo hata baada ya taifa kuingia katika mfumo wa Demokrasia na kurejeshwa vyama vingi vya siasa.
Mwaka 2012, taifa lilianzisha mchakato wa kuandikwa Katiba mpya ya taifa kwa lengo la kutatua matatizo yakiwemo ya uongozi. Rasimu tarajiwa ilipatikana. Rasimu hiyo ilibeba maoni mengi ya wananchi yakiwemo ya kuundwa kwa serikali tatu za Tanganyika, Zanzibar na Muungano. Matarajio yalikuwa Katiba Mpya italeta mfumo mpya wa uchaguzi wenye Tume huru ya uchaguzi.
Pamoja na kila hatua muhimu kukamilika mchakato huo alizimwa, taifa likaingia katika chaguzi zilizojaa majanga. Hivi karibuni taifa linaingia tena katika chaguzi mpya za kitaifa bila ya sheria zenye uwezo wa kutenda haki. Uwezekano wa kutokea mabalaa kama ilivyokuwa katika chaguzi za nyuma ni mkubwa sana.
Kama tulivyosema huko nyuma, matarajio kwa wale waliofunga ni kuyaingiza mafundisho ya Ramadhani katika jamii. Mafundisho hayo yatumike kujenga uongozi bora. Dhamana ya uongozi wapewe wale waadilifu wenye utu na huruma kwa binadamu wenzao. Katu wasipewe watu wasio na hisia za utu kwa wengine.
WAJIBU WA KIJAMII
Elimu ya Uraia
Katika sura ya ‘MAFUNDISHO YA RAMADHANI’ tumeona wajibu wa “Mtu wa Watu”. Katika Sura hii tunaelekeza akili zetu katika uchaguzi mdogo na mkubwa wa kitaifa unaokuja hivi punde.
Kwa hakika Waislamu ni wakongwe wa siasa za Tanganyika na Zanzibar. Fikra na harakati zao ni mchango mkubwa katika uhuru wa mataifa hayo na msingi wa vyama vilivyoleta uhuru vya TANU na ZNP-ZPPP. TANU (Tanganyika Afrikan National Union), ilidai na kupata uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Waingereza mwaka 1961.
ZNP (Zanzibar Nationalist Part), ilidai na kupata uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Waingereza mwaka 1963. ZNP ilitawazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar baada kukishinda chama kikuu cha upinzani ASP na vingine katika uchaguzi wa vyama vingi Julai 1963).
Katika duru za Tanganyika moja ya matukio makubwa ni lile la kuvunjwa kwa Baraza la Wazee wa TANU mwaka 1963. Baraza hilo muhimu la wapigania uhuru liliongozwa na Sheikh Suleiman Takadiri na baadae Mzee Idd Tulio. Lilikua na wajumbe 120, wote Waislamu. Pamoja na changamoto hiyo Waislamu hawakusita waliendelea kushiriki siasa.
Taifa liliporejea katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Maimamu Tanzania waliunda chombo maalum cha kuratibu ushiriki wa Waislamu katika siasa. Chombo hicho KAMATI KUU YA SIASA YA SHURA YA MAIMAMU TANZANIA kimepata umaarufu kwa kutoa Elimu ya Uraia na nyaraka za miongozo.
Katika fursa hii ya Baraza la Idd, Kamati hiyo inatoa pongezi kwa Waislamu kwa kukamilisha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Katika salamu hizo inawajulisha kuwa ipo kazini katika suala la Elimu ya Uraia na itatoa Mwongozo wa namna bora ya Waislamu kushiriki chaguzi za Serikali ya Mtaa na Serikali Kuu zijazo.
WAJIBU WA KIMATAIFA
Palestina Ghaza
Watanzania wengi tunaguswa sana na ukatili wanaofanyiwa binadamu wenzetu huko Gaza Palestina. Unyama dhidi ya ndugu zetu hao wanaopigania haki yao ya uhuru kutoka kwa wavamizi wa Israeli, unafanywa na majeshi ya wavamizi hao.
Israel wakisaidiwa na washirika wao Marekani na mataifa mengine ya Magharibi, mpaka sasa wamekwisha wauwa raia wake kwa waume, vijana, wazee na watoto wasio na hatia zaidi ya 50,000. Majeshi hayo yanayofanya ukatili wa kihayawani, yanavunja Misikiti, Makanisa, Hospitali, Shule, Makazi ya watu na kila jambo baya dhidi ya ubinadamu wanafanya.
Tarehe 11.11.2023, nchini Tanzania wananchi tulipanga kufanya maandamano makubwa ya kulaan ukatili huo dhidi ya ubinadamu. Maandamano hayo yaliyokua na maandalizi makubwa yaliyohusiha bendera nyingi za Palestina, mabiramu makubwa, mabango na mavazi yenye wito wa kusitishwa ukatili na mauwaji, hayakufanyika baada ya Jeshi la Polisi kuyazuia kwa sababu zisizo na mashiko.
Kwa hakika hatuwezi kufunga midomo yetu wakati tunaona na kushuhudia ukatili, mateso na mauaji ya watoto, wanawake na watu wa Gaza yanayoendelea bila ya kuzuiliwa.
Tunatoa wito kwa Wafalme wanaotawala katika mataifa ya Waislamu, wapeleke majeshi Palestina kuzuwia uhalifu wa kimbari unaofanywa na Mayahudi na kuwasaidia Wapalestina kukomboa taifa lao.
Tunatoa wito kwa watu wa mataifa mbalimbali kususia bidhaa za Israel na kuendele na harakati za kupaza sauti. Tuendelee kupeleka misaada ya kibinadamu na kuwaombea dua wanyonge Wapalestina.
Tunatoa wito kwa Serikali yetu ya Tanzania kuheshimu msimamo wa taifa letu wa kuvunja mahusiano yote na mamlaka katili ya Uzayuni wa Israel ulioasisiwa na rais wa kwanza wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
SALAAMU ZETU ZA IDD EL-FITRI ZIWAFIKIE WATANZANIA WOTE
__________________________________
SHEIKH PONDA ISSA PONDA
KATIBU MKUU SHURA YA MAIMAMU TANZANIA