MIMI MJUZI
New Member
- Jan 1, 2016
- 1
- 1
Ndugu zangu salaam. Ni matumaini yangu kwamba harakati za music zinaenda vizuri na bado tunapigana kuweza kufika mbali kimuziki na hatimae siku moja tujulikane.
Natumia muda huu kuandika walaka huu, nikiwa katika hali ya kushangazwa au kushtushwa na tamko la serikali la kutaka wasanii waanze kulipwa kuanzia tarehe 1/1/2016.
Huu ni waraka maalumu kwa wasanii wachanga wote, ukiupata usiache kumtumia na mwingine ili siku moja wewe na mimi tufike tunapotaka kufika.
SERIKALI kupitia waziri wa utamaduni na michezo imetangaza kuwa kuanzia tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka ujao yaani 2016 wasanii watatakiwa kulipwa kwa kila video au audio itakayochezwa kwenye redio au TV stations mbalimbali.
Akiendelea amesema msanii, mtunzi, au producer atapata 60% ya mapato hayo (bongo5 2015).
Hili swala sio baya kwasababu kila msanii awe ndogo au mkubwa anapenda siku moja anufaike kutokana na mziki wake. Swali la kujiuliza je hili swala lina manufaa kwa wasanii wote? (Wakubwa kwa wadogo?) Je serikali imeangalia athari zinazoweza kutokea kwa kuanzisha huu mfumo na wamejiridhisha kwamba faida ni kubwa kuliko hasara?
USHAURI WANGU KWA WASANII.
Kumbuka kuwa media zinafanya biashara na mtu yeyote anaefanya biashara anategemea faida. Kitakachofanyika ni redio na tv zitafanya adjastment ya bajeti zao na kuwalipa wasanii ambao wanajulikana na ambao kupitia wao basi media zitapata faida. Msanii mchanga hautafikiriwa kwenye hili.
Jaribu kujiuliza, zamani ilikuwa bure na hukupewa airtime je sasa wamesema wakulipe utapewa airtime?
zamani tulikuwa tukitumia njia 3 ambazo kupitia hizi, ilimsaidia msanii kujulikana nazo ni
1. media kama redio & TV.
2. Blogs & websites
3. Mtaa kwa mtaa
Kilichofanyika sasa ni kupunguza njia moja ya media, kwa maana nyingine tumebakiwa na njia mbili tu za kutufanya tufikie ndoto zetu.
NAWASHAURI
1. mtumie nguvu nyingi kusambaza nyimbo zenu kupitia BLOGS & WEBSITES ili mtaa uelewe. Mtaa ukielewa utawafanya media wakutafute maana ikumbukwe kuwa media zipo kwaajili ya watu na watu wanachotaka kuona au kusikia ndicho media zinatafuta.
2. Hakikisha kabla hujaachia wimbo wako uwe na bajeti nzuri au connection na blogs & website nyingi ili tu wimbo utakapoachiwa usambazwe kila kona hatimae ufikie point ya media kukulipa. (Maana kulipwa kwasasa sio kazi rahisi)
USHAURI KWA SERIKALI.
1. Hili swala linahitaji muda ili liwe sawa kabisa!
Sina maana ya kwamba mmekurupuka kwenye hili hapana.
Ila ninachokiona ni kwamba mngetumia muda kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa mziki mikoa yote ili mpate picha halisi ya hili swala.
2. jaribuni kuangalia wasanii wachanga hili swala litawaumiza kiasi gani kuliko kuangalia upande mmoja kama mlovyofanya.
Mkumbuke kuwa msanii ili awe mkubwa lazima awe mchanga kwanza. Sasa mkiwapoteza hawa wasanii wachanga mnadhani kwesho ya mziki wa Tanzania ni ipi?
3.Ikumbukwe kwamba mziki umeajiri asilimia kubwa ya vijana (wasanii, watunzi, producers, djs, dancers, directors, bloggers na designers) na wengi wao wanaendesha maisha yao kupitia mziki tu, leo mkianzisha mfumo ambao utaua industry hii mnategemea hawa watu wataishi vipi?
Agalieni msijikute mnaongeza tatzo la ajira badala ya kupunguza.