gnassingbe
JF-Expert Member
- Jun 14, 2015
- 4,826
- 3,577
Habari wandugu ningependa kujuzwa juu ya suala linalonitatiza kuna jirani yangu anaendeleza eneo lake ila shida ni kwamba limejaa mawe makubwa sana sasa alileta mashine ya kupasua siku kadhaa zilizopita zina mikelele lakini sio shida si ndo maendeleo hayo sasa naona hali imekuwa mbaya baada ya kuanza kutumia baruti hapo sasa! vipande vikubwa vya mawe vinaruka hadi kwenye nyumba zetu yaani ni hatari naomba msaada hivi matumizi ya baruti yakoje na jee ni sawa yaani ni "war zone" milipuko,vipande vya mawe vinarushwa umbali kama mita ishirini hadi thelathini maisha ya watoto wetu yapo hatarini.Je ni sahihi kwenye makazi ya watu?