Wapinzani, wapingaji na wapigaji:Comparative analysis

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,188
7,490
Wakuu, kuna vitu vitatu ambavyo kama hatutaweza kuvitofautisha tutapata tabu saba kuelewa mambo.

1. Wapinzani: Hawa ni watu wenye mawazo mbadala. Wakati wote hutoa mawazo yao kwa kujenga hoja nzitona kwa kushawishi kwa kutumia lugha nzuri. Hawa ni viongozi na wako smart sana. Mara zote wana misingi wanayosimamia, na wanampinga yeyote anayeenda kinyume na misingi hiyo na kumuunga mkono yeyote anayefuata misngi hiyo.

2.Wapingaji: Hawa wao hupinga kila kitu kinachofanywa na mwingine. Yaani kwa mfano wanaweza wakuulize kwa nini unatembea badala ya kusimama, ukisimama wanakuuliza kwa nini umesimama badala ya kulala, ukilala wanakuuliza mbona umelala wenzako wanatembea.Kwa kawaida ni vigumu kujua ni nini wanachosimamia.

3. Wapigaji. Hawa wao huunga mkono kila kitu chenye maslahi kwao. Kwa hiyo ukiona anaunga mkono kitu, ujue ananufaika na ukiona anapinga ujue hanufaiki.

ACT ni namba 1. Hapo juu, kama kuna anayebisha atoe hoja, si kupiga makelele.
 
ajabu chama cha upinzani kinapojiona bora kuliko vingine sababu tu wanaingizwa kwenye serikali ya chama tawala!!!
siku zote boss anampenda mtumishi asiye na madhara,anayeona hawezi kutishia kiti chake.,,hongera ACT kwa kupendwa na ccm
 
seriously mnaenda kutekekeza ilani ya ccm na mnajisifu

Act sio wapinzani..tumesema hili miaka yote
 
seriously mnaenda kutekekeza ilani ya ccm na mnajisifu

Act sio wapinzani..tumesema hili miaka yote
Mkuu, tatizo la tanzania si ilani, tatizo ni watu. Kwa mfano hebu nitajie maeneo matano ya kwenye ilani ya ccm ambayo wewe unafikiri ni tatizo, halafu initajie chama ambacho ilani yake inayatatua na ueleze ni kwa vipi. Hebu tuacheni ushabiki usio na kichwa wala miguu.
 
ajabu chama cha upinzani kinapojiona bora kuliko vingine sababu tu wanaingizwa kwenye serikali ya chama tawala!!!
siku zote boss anampenda mtumishi asiye na madhara,anayeona hawezi kutishia kiti chake.,,hongera ACT kwa kupendwa na ccm
ACT ni bora kwa sababu viongozi wamejiwekea misingi ambayo ni bora na wanaifuata na si vinginevyo
 
Eti mtu mfano anajadili katiba ya ccm kisha anaipinga, halafu kumbe wala hajaisoma, yaani anahisi tu
 
Back
Top Bottom