MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Nina wasiwasi na kwa kususiwa uchaguzi mkuu baadae 2020 na wapinzani juu ya madai kua hakuna tume huru ya uchaguzi, kuna uwezekano mkubwa uchaguzi mkuu ukafanyika kama ulivyokua uchaguzi wa Zanzibar march 2016 bila kuhusisha vyama vikuu vya upinzani. Ni kutokana na minong'ono ya muda murefu kua wapinzani hawatendewi haki kwenye uchaguzi kulingana na mfumo wa tume ya uchaguzi ulivyo ambapo wakurugenzi wa halmashauri za wilaya nchini ambao ni makada wa CCM kusimamia uchaguzi ndio wanaoamua mshindi awe nani.
Hii inaweza kua ni fursa pekee kwa kina "ANKO" kupita bila kupingwa maana hata suala la katiba mpya kwanza sio priority, washindani watabaki kina DOVUTWA na yule wa TADEA, bwana yule wa CUF- P hawezi kufika huko japo anatamani sana kufika huko walao awe mshindani pekee wakati huo, Zitto na ACT yake wataungana na wanaUkawa kuidai tume huru ya uchaguzi japo naye bado kuna wasiwasi akaungana na bwana yule wa CUF-P.
Ni wakati sasa serikali kulipitia jambo hili mapema kabla ya muda kufikia huko, mambo kama haya hua sio mazuri sana na yanaweza kuleta malumbano yasiyokua na msingi wowote nchini. Kwa wapinzani hawa wa sasa hasa wanaUkawa sidhani kama kuna mtu atakubali kuingia kwenye uchaguzi 2020 kwa tume hii.
Haya ni maoni na fikra zangu, lakini muda ni hakimu mzuri sana.