Wapinzani wanajitoa mwali wenyewe,wanajialika,wanajipigia ngoma,wanacheza na kujituza wenyewe.

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Nmekuwa nikijiuliza ni lini staili ya kususa iliwah wasaidia waafrika popote pale?hasa huku kwetu pwan wanasema" yakhe ukisusa siye twala" suala la kumsusia Dr Tulia bunge kiuhalisia lina athar gan kwa serikal au ccm? Lakini ni kwel leo hii tulia ni mbabe kuliko alivyosemwa ndugai awam iliyopita?mpaka kusema alikuwa ameathiria na bhang ashakum si matusi.
Ni mara ngap wapinzan wamesusa na hatujaona athari yoyote?

Walisusa zanzibar dr shain akapita nakuapishwa kuwa rais na nch inaendelea.

Walisusa bunge la katiba na ndugu mmoja akasema ccm ni intarahamwe baadaye akaja kutumika nao hao hao. Na bunge likapitisha katiba elekezi mbovu kabisa duniani.

Wamesusa kwa mambo mbalmbal yakapita kama kawaida pasipo athar yoyote. Sasa hivi wamempaisha sana dr tulia kwa sabab ambazo hazina msing.kumbe wangemdharau tu ingetosha wachukulie kama pale mbele hamna kitu.

Lakini najiuliza ukiwa umelima shamba lako wataka vuna kabla ya mavuno nyani wanaiba mazao. Unapambana nao kwa njia hii wanakushinda kwa kuja kuiba usiku. Unaamua kususa kiwaachia shamba.

Ccm wanafurah mnaposusa.maana wao ndo wala. Nadhan kuna haja ya kutafuta njia mbadala zaid ya kususa.kama si hivyo mtajukuta ninyi wenyewe ndo wali,mnajiamualia kujitoa ndani,mnajialika wenyewe,mnapiga ngoma na kucheza wenyewe halafu mnatuzana pesa kwa bashasha kabisa ambazo ni pesa zenu wenyewe. Leo hii hata kikwete amekuwa mwema kwenu, ndugai amekuwa mwema kwenu.mwaka 2020 akija mwngne watasema tunamkumbuka dr tulia alikuwa hatufanyii ubabe kama hyu.
 
ukawa hawataki kula wala kushiri haramu!ccm wale na hakuna anae wazuia...najisi hatuwezi shiriki!
 
Back
Top Bottom