ANKOJEI
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 996
- 743
Takribani miezi kadhaa baada ya Magufuli kushinda uchaguzi kwa matokea ambayo yalitegemewa kugomewa na vyama vya upinzani endapo mshindi yeyote wa CCM angeshinda, SASA wapinzani wake ambao si wa kisiasa bali wa kisera na kiuchumi wameanza kujitokeza.
Baada ya siku 60 za kuchaguliwa kwake wapinzani wengi walikaa kimya hasa kusubiria uchaguzi wa baraza la mawaziri lakini Magufuli aliwapiga chenga na kuendelea kupiga kazi Muhimbili, Bandarini na TRA pamoja na TRL. Wengi hawakujua nini hasa mbinu za Magufuli katika kuhakikisha anatimiza ahadi zake.
Siku za hivi karibuni yameibuka maswali mengi lakini makubwa ni:
1. Je Magufuli ana mbinu na uwezo wa KUKUZA UCHUMI (ECONOMIC GROWTH STRATEGY)
2. Je kubana kabisa na kufuata sheria za kodi 100% ni njia sahihi na ya Kudumu? (SUSTAINABLE)
3. Je mfumo wa serikali na chama cha CCM uliotufikisha hapa utaweza tena kwenda na (COMPATIBILITY)
Ndipo nikalazamika Kuangalia Clinton alifanya nini?
Clintoni aliingia Madarakani na kukuta Uchumi wa Marekani ulio mbovu kabisa, nini alikifanya?
1. Kusimamia mapato na matumizi ya serikali na hivyo kufuta nakisi ya bajeti na kuhakikisha serikali inajitegemea kibajeti bila kukopa kopa ovyo.
2. Hivyo serikali ilipata pesa ya kulipa deni la Taifa lililokuwa kubwa
3. Kuunda sheria ya kazi na ujira kwa wasio na kazi pia wasiojiweza na waleao watoto katika mazingira magumu
4. Kupunguza riba za mikopo
5. Kuweka ukomo wa mfumuko wa bei
6. Kufungua milango ya uwekezaji toka nje ya nchi
6. Kuwekeza katika mtaji wa watu, elimu na ufundi pamoja na utafiti
7. Kulipisha kodi kubwa kwa matajiri na kupunguza kwa maskini
Matokeo yake uchumi wa Marekani ulifurika haraka sana
1. Deni la taifa lilipungua
2. Uchumi ulianza kukua tena
3. Ajira zikawepo
4. Wagunduzi na watafiti wakaongezeka
Nashawishika mambo Mengi aliyoyafanya Clinton yanashabiana na Magufuli ndio mana nasema ni Clinton mpya wa Africa.
Sasa tukirudi katika maswali haya matatu,
1. Je anao uwezo wa KUKUZA UCHUMI (ECONOMIC GROWTH STRATEGY)
2. Je kubana kabisa na kufuata sheria za kodi 100% ni njia sahihi na ya Kudumu? (SASTAINABLE)
3. Je mfumo wa serikali na chama cha CCM uliotufikisha hapa utaweza tena kwenda na KASI HII YA MAGUFULI
Wataalamu wanasema ili nchi za Africa zipate kuondokana na Umaskini basi uchumi wake lazima ukue katika kiwango cha zaidi ya asilimia 10 yaani double digit growth. Kama Magufuli hataifumua mifumo inayozuia ukuaji wa uchumi kwa kasi pamoja na kukibana chama chake basi huenda tukabakia na uchumi wa chini ya 10%. Pia kuna uharaka wa dola kufikia 1800 na baada ya hapo iendelee kushuka ili wanachi wafurahie ukuaji wa uchumi wao.
Ingawa wapinzani hawa wameanza mapema kupiga za chinichini mimi binafsi nawaunga mkono lakini napendekeza kuwe na midahalo ya wazi kumshauri rais nini afanye ili kukuza uchumi wetu. Atahitaji pia kuwa na washauri wa kiuchumi imara ambao si wanasiasa.
Kama wewe ni mjasiriamali basi unaweza kuchungulia sekta kadhaa zinazoonyesha matarajio ya kukua kwa haraka sana ndani ya miaka 5 ya utawala wa magufui hapa chini.....
Price Watch Afrique: MAGUFULIFICATION: CLINTON MPYA AFRICA
Na pia ukitaka kujua nini Magufuli amekifanya ndani ya siku 60 za utawala wake bofya hapa
Price Watch Afrique: SIKU 60 ZA UTAWALA WA MAGUFULI
Swali linabakia "ATAKUZA UCHUMI?