Wapinzani Vs Dr Magufuli

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
1,984
1,405
Katika kitabu takatifu biblia kuna mwandishi moja aitwaye Paulo, mwinjilisti Paulo ambaye anajitambulisha kuwa ni Myahudi kwa wayahudi, Mebrania kwa Waebrania na Myunani kwa Wayunani ameandika vitabu vingi ktk agano la jipya, Paulo ambaye alikuwa msomi mzuri ktk nyakati hizo maandiko yake mpk leo imewachanganya wasomi wa Elimu Mungu (Theology) kutokana upeo na IQ yake ilivyokuwa kubwa Maandiko hayo Paulo yamewachanga wanatheolojia wengi duniani na kila kundi limetafsiri maandiko ya Paulo kadri walivyofikiri wao na wengine kupotosha wafuasi wao ili uweze kumuelewa Paulo unapaswa kusoma na kutafakari maandiko yake kwa hekima kubwa kuliko kawaida, wanatheolojia wanamsemo wao uitwao uvuvio, Paulo msomi wa ngazi ya PhD ktk Elimu ya Kiyahudi mjumbe wa baraza la kiungozi la kiyahudi mwanasheria mkuu wa baraza na mtalaam wa elimu Mungu anapoandika waraka zake kwa mataifa mbalimbali anatumia lugha sadifu ya kiebrania na pia kiyunani amewachanganya watu wengi wasomi wa nyakati hizi wakati mwingine alitumia maneno makali sana lakini lengo lake kuu ilikuwa ni watu kumtambua Bwana Yesu na wafike Mbinguni. Nyakati hizi kuelekea 2025 tanzania tumebahatika kumpata Rais mwenye upeo na maono makubwa kwa Taifa letu, Rais mzalendo asiyepoteza muda na porojo na ulaghai Mwanafalsafa aliyesoma vizuri na kuhitimu elimu ya falsafa kama Paulo wa kwenye biblia, amekuwa akitoa matamko yanayochanganya wapinzani ili kumwelewa mh Dr John Pombe Magufuli inakubidi uwe IQ kubwa ambao wenzetu wanatheolojia wanauita Uvuvio watu wenye upeo wa gumbaru km akina Mbowe, Lema, Msigwa, Saed, waitara, James,Magdalina, mtatiro, heche,nk wameshindwa kumwelewa mh rais kwa uwezo wa kutafakari ni mdogo, IQ haipatikani kwa kusoma darasani bali ni uwezo unaopatiwa na Mwenyezi Mungu kukusaidia kutambua na kufikiri zaidi. Mh Rais alipoongea siku akipokea ripoti ya NEC alipoomba kushirikiana na wapinzani ktk mitaa yao, kata zao, majimbo yao ili wasimamie watendaji wa serikali kujiletea maendeleo na kutimiza kile walichoombea kura Wapinzani wao wakadhani wamezuiliwa kufanya siasa make wao kwa siasa ni kuzurura na kutapanya ruzuku kwa posho na siyo kuwatumikia wananchi waliowachagua kuanzia ngazi ya vijiji, mitaa, kata, majimbo bali kuzurura tu. Mh Rais aliposema anatumbua majipu kupambana na ufisadi waowalitafsiri Rais anawaonea mafisadi akili zao zimewapeleka kwa fisadi wao mkuu namba moja wa nchi wakidhani atatumbuliwa na tonge kuwaponyoka mdomoni, juzi mh Rais aliposema atawalinda wastaafu wakakimbilia kudhani atakayelindwa ni kikwete, Mkapa, Mwinyi na akina Waryoba wakasahu kuwa nawao pia wanao wastaafu akina Edward Lowassa, Fredrick Sumaye na mzee Ngombale Mwiru ambao pia wametumikia nchi, hawa wapinzani kumwelewa Magufuli wanahitajika wapate uvuvio ya aina take kwakuwa jamaa amewazidi upeo na maarifa. Muda sasa umefika unahitajika upinzani wenye maarifa na itikadi pambanishi upinzani wenye siasa za ushindani siyo upinzani wenye kutafuta ruzuku ili waishi kwa mantiki hiyo ndiyo sasa nawaona Prof Ibrahim Lipumba na Prof Kitila Mkumbo wabobezi wa fikra ktk hitaji la siasa za sasa ktk vyama vya upinzani ili kujenga upinzani imara. Mungu umpe Fadhili nyingi Dr JohnPombe Magufuli, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chama cha Mapinduzi make bila ccm imara nchi itayumba.na Frey Cosseny
 
Back
Top Bottom