Wapinzani tuache ndoto za mchana

Wapinzani tuache ndoto za mchana

Gheto's King

Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
11
Reaction score
0
Kumekua na upotoshaji Wa ajabu unaofanywa na upinzani katika kiwango kisichoelezeka. Wanatuambia mwaka 2015 waliibiwa kura za uraisi, OK tu assume kuwa kweli mliibiwa kura za uraisi hivyo mlishinda uraisi, sasa tuje katika upande Wa viti vya ubunge, mlishinda vingapi kulinganisha na Chama tawala? Hivi kwa idadi hii ya wabunge mliyonayo, mngepewa uraisi hivi Lowasa angetawala kweli kwa Amani kama Si kwenda kumzeesha Mzee Wa watu, mana angekumbana na upinzani Wa kutosha kutoka bungeni na asingeweza kufurukuta tuwe Wa kweli katika hilo. Nini suluhisho LA upinzani Tanzania? Jambo LA msingi kabisa kama kweli MNA dhamira ya dhati ya kusaidia taifa hili hebu achaneni na ndoto ya kiti cha uraisi, tafuteni viti vya kutosha bungeni ili muweze kupitisha sheria ambazo automatically zitambana raisi then hapo ndipo mtakua na nguvu ya kuwania hicho kiti, kwa sasa sheria za nchi zitaibeba chama tawala miaka nenda rudi mana wao ndio kwenye maamuzi bungeni, mfano mzuri tunaona ishu ya bunge LA east Africa mambo yalivyokua, so ushauri wangu ni kua upinzani hebu uache kuwekeza nguvu nyingi kwenye uraisi ambao kimantiki utakua ni sawa na mbwa aliyevikwa lijamu, Bali uwekeze ktk utafutaji viti Vingi vya ubunge ili uwe na nguvu ya kura ya maamuzi bungeni, hapo ndipo tutakapoona Tanzania mpya vinginevyo mtakuwa wale wale Wa kutaka madaraka tuu wala hamna jipya.
 
Back
Top Bottom