Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,547
- 47,198
Baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari, wakati nasubiri kujinga na elimu ya juu, kulikua na kama miezi 8 au tisa hivi ya kusubiri, nikaona kuliko kukaa bure wacha nijishughulishe, nikajiunga na chuo cha uandishi wa habari kwa mafunzo ya miezi sita.
Wakati nikijifunza uandishi wa habari nikadevelop interest ya kujifunza kupiga mziki redioni na clubs wanaita maDJ kipindi kile tulikua na majina tunawapa maDJ wanaopenda kupiga nyimbo zinazowika tu kwa kipindi kile ili kujizolea umaarufu, maDJ matunda yaani anachagua zile nyimbo nzuri zoote anazipiga ili wasikilizaji waone anafanya kazi nzuri kumbe ubora wa DJ ni kupangilia miziki kwa kufuatana na kiki, mashine tuliyokua tukitumia kipindi kile ilikua inaitwa denon.
Mantiki ya kuwapa historia fupi ni katika kutaka kupalilia dhana na matumizi ya neno "matunda" nikihusianisha na jinsi wapinzani hapa nchini wanavyoendesha siasa zao.
Wanasiasa wa upinzani wengi wao hawana uwezo wa kuibua mijadala na kuifanya mijadala ya kitaifa , bali hudandia matukio na kuyafanya kama yao kuyajengea hoja na kujiongezea umaarufu. Hili limekua jambo la kawaida kabisa.
Ndio maana mijadala kama Richmond, Escrow na mingineyo bado haijafungwa kwakua wanasiasa wetu hawana uwezo wa kuibua hoja nyingine zaidi ya kuibua mambo yale yale yanayovutia masikioni mwa watu ili wabakie kwenye headlines za vyombo vya habari.
Matatizo katika taifa hili yapo mengi, hakuna maji, hakuna dawa, elimu ni mbovu, bei za mafuta zipo juu, mishahara midogo nakadhalika nakadhalika, lakini kwa ajabu la wengi hoja zinazozungumziwa na wanasiasa wetu kwa kipindi cha takribani miaka kumi, ni mbili tu RICHMOND na ESCROW.
Jamani wanasiasa wetu, tutafute namna ya kuzimaliza hizo hoja mbili hapo juu, na kwenda moja kwa moja kwenye matatizo yanayotukumba sisi wapigakura wenu moja kwa moja, ukimuuliza mama muuza nyanya kama anafahamu IPTL au Richmond kwa undani wake sidhani kama atakuelewa, ingawa hoja zinajengwa ilikuonekana kama RICHMOND na ESCROW pekee ndio vyanzo vya kila tatizo hapa nchini sidhani kama ni kweli.
Kuna haja ya kujitazama upya na kuibua hoja za kujenga taifa sio kufanya siasa matunda kwa kudandia hoja zinazovuma.
Wasalaam.