Wapinzani Kuendelea Kucheza Kwenye Mikono ya CCM

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Bila wapinzani kupanga mikakati ya pamoja wataendelea kucheza katika mikono ya CCM. Wakati wa uchaguzi mkuu uliopita baada ya vyama kuingia kwenye uchaguzi kwa kutumia mwamvuli wa Ukawa ushindi mkubwa ulipatikana katika kura ya urais. Majuzi kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe alitoa kauli kali dhidi ya serikali ya awamu ya tano lakini baada ya mwanasiasa wa chama hicho kuteuliwa kuwa Katibu mkuu wa wizara ya maji huyo huyo Zitto Kabwe ameanza kusifia serikali. Chama cha CUF ndio kwasasa mgogoro mkubwa unaendelea kati ya Lipumba na Seif Sharrif Hamad ni hii dalili mbaya.
Watanzania wanataka mabadiliko na bila kuwa na chama imara CCM haiwezei kuondoka madarakani, kinachotakiwa ni mikakati ya mapema kupangwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020, mfano katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Kenya vya siasa vya Kenya vimeunda National Super Alliance (NASA) kwenye hii NASA kuna Muungano wa vyama ODM, Wiper, Amani na Ford Kenya na vyama vyote vimesaini Memorandum of Understanding jinsi watakavyo gawana madaraka baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu.
CCM inapoona umaarufu wake unashuka huwa wanakimbilia kutoa nafasi kwa upinzani kujiunga na serikali ili kurudisha imani ya wananchi kwenye chama hicho, ni wakati muhimu kwa haswa chama kikubwa cha upinzani cha Chadema kukomazaa demokrasia ndani ya chama halafu kuanza kuweka mikakati ya kuunda ushirikiano na vyama vingine.
Bila kufanya hivyo mtawavunja nguvu Watanzania wenye kiu ya mabadiliko.
 
Washauri kwanza chadema waache ubinafsi na wajifunze maana ya Demokrasia ukawa imeuliwa na chadema kwa kutokuwaheshimu wengine na kutaka kila kitu kiwe chao!
 
Washauri kwanza chadema waache ubinafsi, ukawa imeuliwa na chadema kwa kutokuwaheshimu wengine na kutaka kila kitu kiwe chao!

Naona Kuna Bashite huko EALA sijui mlimpitishaje maana Majigambo yote ya Jana kumbe hamna kitu.
 
Washauri kwanza chadema waache ubinafsi, ukawa imeuliwa na chadema kwa kutokuwaheshimu wengine na kutaka kila kitu kiwe chao!
Huo ni ukweli kama nafasi moja wangeitoa kwa CUF A ya Seif wangeonyesha uzalendo wa hali ya juu. Mgombea urais wa Chadema alipata kura nyingi Zanzibar kupitia mgongo wa CUF.
 
Back
Top Bottom