Wapigania Uhuru wa Tanganyika wanaosubiri kutambuliwa wakiwa Makaburini

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,806
31,823
tAZ7Q0CbeIpy9U9VrFhQRXVT3KiZoLVWyGRWVQGRN9MQ2MWqQTn6Pdw3hADo7z3DvALdD5Hr-xQ=w724-h567-no

Wazee wa Dar es Salaam katika Baraza la Wazee wa TANU na Mwalimu Julius Nyerere katika Uchaguzi Mkuu wa 1962.

Masikitiko ni kuwa mashujaa hawa hadi leo nchi haijawatambua isipokuwa Nyerere peke yake.

Kushoto ni Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana, Julius Nyerere na Mshume Kiyate picha ilipigwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 1962.​
 
Ulitaka tuwakumbukaje mkuu?
Mchapafito,
Ningefurahi sana kama tungewakumbuka kwa kuipa mitaa majina yao
kama vile Mtaa wa Tandamuti ulivyobadilishwa na kuitwa Mtaa wa
Mshume Kiyate.

Huu ni mfano mmoja.

Jengo la CCM ambalo ndipo yalipokuwa makao Makuu ya African
Association na ndipo palipokuja kuasisiwa TANU nyumba hii ilijengwa
kati ya mwaka wa 1929 - 1933 na ilijengwa kwa kujitolea na viongozi
wa wakati ule.

Baadhi ya viongozi hawa walikuwapo hadi TANU ilipoasisiwa lakini leo
ukiingia katika ofisi za CCM hakuna hata kumbukumbu ya picha zao mle
ndani.

Ikiwa Bunge Dodoma kuna Ukumbi wa Msekwa kwa heshima ya mchango
wake katika Bunge kwa nini leo tusiwa na ukumbi wa mkutano katika ofisi
kwa kumbukumbu ya Abdulwahid Sykes au Earle Seaton au Sheikh
Hassan bin Amir
au Sheikh Suleiman Takadir.

Ikiwa labda wewe hujapatapo kusikia majina hayo katika kupigania uhuru
wa Tanganyika nakushauri usome kitabu cha Abdulwahid Sykes.

Ukipenda zaidi ingia hapa:
Mohamed Said: KUTOKA JF: ATHARI YA KUJARIBU KUIBADILI HISTORIA YA TANU NA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
 
Mchapafito,
Ningefurahi sana kama tungewakumbuka kwa kuipa mitaa majina yao
kama vile Mtaa wa Tandamuti ulivyobadilishwa na kuitwa Mtaa wa
Mshume Kiyat

Huu ni mfano mmoja.

Jengo la CCM ambalo ndipo yalipokuwa makao Makuu ya African
Association na ndipo palipokuja kuasisiwa TANU nyumba hii ilijengwa
kati ya mwaka wa 1929 - 1933 na ilijengwa kwa kujitolea na viongozi
wa wakati ule.

Baadhi ya viongozi hawa walikuwapo hadi TANU ilipoasisiwa lakini leo
ukiingia katika ofisi za CCM hakuna hata kumbukumbu ya picha zao mle
ndani.

Ikiwa Bunge Dodoma kuna Ukumbi wa Msekwa kwa heshima ya mchango
wake katika Bunge kwa nini leo tusiwa na ukumbi wa mkutano katika ofisi
kwa kumbukumbu ya Abdulwahid Sykes au Earle Seaton au Sheikh
Hassan bin Amir
au Sheikh Suleiman Takadir.

Ikiwa labda wewe hujapatapo kusikia majina hayo katika kupigania uhuru
wa Tanganyika nakushauri usome kitabu cha Abdulwahid Sykes.

Ukipenda zaidi ingia hapa:
Mohamed Said: KUTOKA JF: ATHARI YA KUJARIBU KUIBADILI HISTORIA YA TANU NA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

You should be ashamed of yourself. Lot of people did and so much more are still doing great job for this great nation but that shouldn't be taken as a criterion for unnecessary entertaining cheap exeptionalism. its shame for a person of your age, under the influence of religious prejudice, periodically attempting to illegitimately impose your selfish needs and desires on others. If those people fit your criteria for heroism why cant you keep it private since you independently perceive them as such? The history has already been written, MOVE ON.
 
Nakumbuka kauli ya hayati baba wa taifa kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha rasmi ya taifa na dhumuni kubwa ni kuifanya ivuke mipaka zaidi ya Tanzania...unapoandika kiingereza na wakati mleta Uzi ameandika kiswahili inaonesha wazi namna ulivyo limbukeni wa lugha ya malkia. Kuna forum za kiingereza nyingi tu changia kwa lugha hiyo, inaonesha wazi umesoma maelezo fika na kuelewa kisha kwa utashi wako ukaona ubadili lugha ili sijui ueleweke sana au iweje Unajua wewe na nafsi yako...soma alama za nyakati sio kila mahala pa kuandika lugha ya malkia ndugu, hivyo mara nyingine jifunze kuandika kwa lugha ya taifa mahala panapostahili na kiingereza mahala panapostahili....
 
hivi kushiriki katika uchaguzi na kupiga Picha na aliyeshinda hicho kinakuwa kiashiria cha ushujaa(kupigania Uhuru). mzee Mohamed Said ni vena ungeonesha mchango wao ktk harakati za Uhuru badala ya kutuwekea Picha na kutaka kutuaminisha kwamba wana mchango mkubwa ktk taifa hili
 
Uhuru n Umoja,
Sijui kwa nini umehamaki na kuja na vitisho vya Kiingereza.

Ninakujibu kwa Kiswahili kwa kuwa sitaki nami niwe kama wewe
kujigeuza mfungwa bila sababu.

Nina Merit (First Class Pass) Cambridge English Oral Cambridge
Examination 1970.

Nimeshirikishwa na Oxford University Press Nairobi kuandika vitabu
vya kiada vyaa kusomesha lugha ya Kiingereza na nina vitabu viwili
viko katika mtaala Kenya.

Kazi hizi zimefanywa 2006 na 2007.

Kiingereza nakijua vizuri sina ushamba wa kutaka watu wanijue kuwa
mimi ni mtaalamu wa lugha hiyo.

Nimechapa kitabu cha Abdul Sykes kwa Kiingereza London (1998)
na pia nimeshiriki kama mmoja wa waandishi wa Dictionary of African
Biography (DAB), Oxford University Press, New York (2011).

Naamini tushaelewana.
 
Nakumbuka kauli ya hayati baba wa taifa kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha rasmi ya taifa na dhumuni kubwa ni kuifanya ivuke mipaka zaidi ya Tanzania...unapoandika kiingereza na wakati mleta Uzi ameandika kiswahili inaonesha wazi namna ulivyo limbukeni wa lugha ya malkia. Kuna forum za kiingereza nyingi tu changia kwa lugha hiyo, inaonesha wazi umesoma maelezo fika na kuelewa kisha kwa utashi wako ukaona ubadili lugha ili sijui ueleweke sana au iweje Unajua wewe na nafsi yako...soma alama za nyakati sio kila mahala pa kuandika lugha ya malkia ndugu, hivyo mara nyingine jifunze kuandika kwa lugha ya taifa mahala panapostahili na kiingereza mahala panapostahili....

Achana nae huyo ni mtumwa wa lugha za watu lugha ya mama yake yenyewe hajui
 
hivi kushiriki katika uchaguzi na kupiga Picha na aliyeshinda hicho kinakuwa kiashiria cha ushujaa(kupigania Uhuru). mzee Mohamed Said ni vena ungeonesha mchango wao ktk harakati za Uhuru badala ya kutuwekea Picha na kutaka kutuaminisha kwamba wana mchango mkubwa ktk taifa hili
Lutayega,
Umekosea kusema.
Ulitakiwa wewe kuuliza kwani Kiyate Mshume ni nani?

Sasa mimi ningekueleza mchango wa Mzee Kiyate kwa
Nyerere na TANU wakati wa kudai uhuru.

Nina hakika ungeshangazwa.
Ingia hapa:
 
Nilivyoona tu kichwa cha habari, nilijua wewe ndio mleta mada... Toka ulete mada ile ya mtoa taarifa aliyekuzaa... Nina mashaka na hawa pia wanaotafuta kutukuzwa kwa sasa.
 
Uhuru n Umoja,
Sijui kwa nini umehamaki na kuja na vitisho vya Kiingereza.

Ninakujibu kwa Kiswahili kwa kuwa sitaki nami niwe kama wewe
kujigeuza mfungwa bila sababu.

Nina Merit (First Class Pass) Cambridge English Oral Cambridge
Examination 1970.

Nimeshirikishwa na Oxford University Press Nairobi kuandika vitabu
vya kiada cha kusomesha lugha ya Kiingereza na nina vitabu viwili
viko katika mtaala Kenya.

Kazi hizi zimefanywa 2006 na 2007.

Kiingereza nakijua vizuri sina ushamba wa kutaka watu wanijue kuwa
mimi ni mtaalamu wa lugha hiyo.

Nimechapa kitabu cha Abdul Sykes kwa Kiingereza London (1998)
na pia nimeshiriki kama mmoja wa waandishi wa Dictionary of African
Biography, Oxford University Press, New York (2011).

Naamini tushaelewana.

Mimi nakufahamu vizuri, vizuri sana, na nakufuatilia vyema, nlikuona kwenye moja ya university USA but sikumbuki wapi niliona picha ile.

"sina ushamba wa kutaka watu wanijue kuwa
mimi ni mtaalamu wa lugha hiyo."

Hii ni ajabu sana, na kwa kina naona unahamaki na hutaki ongelea ujumbe niliokufikishia.

Matumizi ya lugha sio ushamba ila ni ushamba kusema matumizi ya lugha ni ushamba. Lugha ni mawasiliano, ingekua vibaya kwangu kutumia lugha ya hiyo kwa asiye na ufahamu, ila kwakua nakufahamu, na najua kua utanipata nliamua kukufikishia UJUMBE kwa lugha hiyo.

Ulichokifanya ni ujanja ujanja wa kukwepa ujumbe maridhawa nliokufikishia na kuamua kuongea ishu za lugha.
 
Nakumbuka kauli ya hayati baba wa taifa kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha rasmi ya taifa na dhumuni kubwa ni kuifanya ivuke mipaka zaidi ya Tanzania...unapoandika kiingereza na wakati mleta Uzi ameandika kiswahili inaonesha wazi namna ulivyo limbukeni wa lugha ya malkia. Kuna forum za kiingereza nyingi tu changia kwa lugha hiyo, inaonesha wazi umesoma maelezo fika na kuelewa kisha kwa utashi wako ukaona ubadili lugha ili sijui ueleweke sana au iweje Unajua wewe na nafsi yako...soma alama za nyakati sio kila mahala pa kuandika lugha ya malkia ndugu, hivyo mara nyingine jifunze kuandika kwa lugha ya taifa mahala panapostahili na kiingereza mahala panapostahili....

Kwenye forum yeyote na kwenye mada yoyote wachangiaji ni wengi hivyo sio lazima kila achangiae humu akupendeze wewe or afanye unachotarajia. ujumbe wangu mimi ni kwake yeye Mohamed Said.
 
Mimi nakufahamu vizuri, vizuri sana, na nakufuatilia vyema, nlikuona kwenye moja ya university USA but sikumbuki wapi niliona picha ile.

"sina ushamba wa kutaka watu wanijue kuwa
mimi ni mtaalamu wa lugha hiyo."

Hii ni ajabu sana, na kwa kina naona unahamaki na hutaki ongelea ujumbe niliokufikishia.

Matumizi ya lugha sio ushamba ila ni ushamba kusema matumizi ya lugha ni ushamba. Lugha ni mawasiliano, ingekua vibaya kwangu kutumia lugha ya hiyo kwa asiye na ufahamu, ila kwakua nakufahamu, na najua kua utanipata nliamua kukufikishia UJUMBE kwa lugha hiyo.

Ulichokifanya ni ujanja ujanja wa kukwepa ujumbe maridhawa nliokufikishia na kuamua kuongea ishu za lugha.
Uhuru n Umoja,
Kuhamaki si hulka yangu na hili lina ushahidi hapa Majlis hata wale
wasionipenda watakupa ukweli huu.

Nilikuwa nataka kwanza tuelewane ndipo tuje katika mnakasha.
Sikuwa nimekwepa ujumbe wako.

Sikimbii mjadala.
Unasema historia ishaandikwa.

Hebu nipe majina ya hivyo vitabu au kitabu ambacho historia ya uhuru
wa Tanganyika na historia ya TANU imeandikwa.
 
Acha udini mzee....binafsi nakuheshimu sana
Mchapito,
Ikiwa unataka kujua kuhusu udini nakuomba usome vitabu hivi:
  1. P van Bergen: Religion and Development in Tanzania (1981)
  2. John Sivalon: Kanisa Katoliki na Siasa Tanzania Bara (1992)
  3. Mustafa Hamza Njozi: Mwembechai Killings (2002)
Katika vitabu hivyo hapo juu kuna mengi ya kujifunza na utajua
hili tatizo lilianza wakati gani na walengwa walikuwa ni kundi gani
katika jamii.

Kitabu cha Njozi serikali wakati wa Mkapa ilikipiga marufuku kwa
kuwa aliyosema kwa ushahidi yalikuwa yanatisha.
 
Mimi nakufahamu vizuri, vizuri sana, na nakufuatilia vyema, nlikuona kwenye moja ya university USA but sikumbuki wapi niliona picha ile.

"sina ushamba wa kutaka watu wanijue kuwa
mimi ni mtaalamu wa lugha hiyo."

Hii ni ajabu sana, na kwa kina naona unahamaki na hutaki ongelea ujumbe niliokufikishia.

Matumizi ya lugha sio ushamba ila ni ushamba kusema matumizi ya lugha ni ushamba. Lugha ni mawasiliano, ingekua vibaya kwangu kutumia lugha ya hiyo kwa asiye na ufahamu, ila kwakua nakufahamu, na najua kua utanipata nliamua kukufikishia UJUMBE kwa lugha hiyo.

Ulichokifanya ni ujanja ujanja wa kukwepa ujumbe maridhawa nliokufikishia na kuamua kuongea ishu za lugha.
Kumbuka lakini hapa tunapitia wengi,kama ujumbe wako wa English umemlenga yeye unge m pm.
 
Back
Top Bottom