Wapi nitapata vitabu hivi?

Franco Zetta

JF-Expert Member
Nov 3, 2014
1,661
843
Wadau, natumaini niko sahihi kuulizia hitajio langu hapa nikiamiani ni jukwaa la watu wapevu walioshiba miaka. Ninahitaji maelekezo ya wapi nitaweza kupata vitabu nitakavyoorodhesha hapo chini ili kumsaidia kijana wangu.

Nimempeleka shule ya English medium na kiswahili kimemponyoka imekuwa ni tatizo kwake kwenye somo hilo darasani. Nikakumbuka nilipokuwa primary miaka ileeee tulikuwa na wakati wa kujisomea vitabu vya hadithi ni vikatujenga sana tu.

Vitabu kama alfu lela ulela 1-4 hivi nilivipata Mkuki publishers,vingine ni

1.Malimwengu (1-12)
2.Sultani Zuwera
3. Mzimu wa Watu wa kale
4.Kisiwa cha Hazina
5.Hadithi za Hazina binti Sultani
6.Adili na nduguze
7.Hadithi za Allan Quaterman
8.Hekaya za Abunwasi
9.Mashimo ya Mfalme Suleiman
10.Lila na Fila havi tangamani
11.Alice katika nchi ya ajabu,

Kwa uchache ni hivi tu japo visipatikane vyote,nitashukuru kwa maelekezo nitakayopata.
 
Wadau, natumaini niko sahihi kuulizia hitajio langu hapa nikiamiani ni jukwaa la watu wapevu walioshiba miaka,nina hitaji maelekezo ya wapi nitaweza kupata vitabu nitakavyo orodhesha hapo chini ili kumsaidia kijana wangu niliye mpeleka shule ya English medium na kiswahili kime mponyoka imekuwa nitatizo kwake kwenye somo hilo darasani,nikakumbuka nilipo kuwa primary miaka ileeee tulikuwa na wakati wa kujisomea vitabu vya hadithi ni vikatujenga sana tu,vitabu kama alfu lela ulela 1-4 hivi nilivipata Mkuki publishers,vingine ni 1.Malimwengu (1-12) 2.Sultani Zuwera3. Mzimu wa Watu wa kale 4.Kisiwa cha Hazina 5.Hadithi za Hazina binti Sultani 6.Adili na nduguze 7.Hadithi za Allan Quaterman 8.Hekaya za Abunwasi 9.Mashimo ya Mfalme Suleiman 10.Lila na Fila havi tangamani 11.Alice katika nchi ya ajabu, kwa uchache ni hivi tu japo visi patikane vyote,nita shukuru kwa maelekezo nitakayo pata.
 
Mkuu hivi vitabu si vya mtoto labda vyako mwenyewe sababu ni vya kale sana
 
Usisahau pia kutafuta cha bulicheka na malkia lizabeta, ni kizuri sana kwa mtoto. Bila kusahau cha similizi za esopo, hicho kimejaa hadithi fupi zenye methali murua.
 
Wadau, natumaini niko sahihi kuulizia hitajio langu hapa nikiamiani ni jukwaa la watu wapevu walioshiba miaka,nina hitaji maelekezo ya wapi nitaweza kupata vitabu nitakavyo orodhesha hapo chini ili kumsaidia kijana wangu niliye mpeleka shule ya English medium na kiswahili kime mponyoka imekuwa nitatizo kwake kwenye somo hilo darasani,nikakumbuka nilipo kuwa primary miaka ileeee tulikuwa na wakati wa kujisomea vitabu vya hadithi ni vikatujenga sana tu,vitabu kama alfu lela ulela 1-4 hivi nilivipata Mkuki publishers,vingine ni 1.Malimwengu (1-12) 2.Sultani Zuwera3. Mzimu wa Watu wa kale 4.Kisiwa cha Hazina 5.Hadithi za Hazina binti Sultani 6.Adili na nduguze 7.Hadithi za Allan Quaterman 8.Hekaya za Abunwasi 9.Mashimo ya Mfalme Suleiman 10.Lila na Fila havi tangamani 11.Alice katika nchi ya ajabu, kwa uchache ni hivi tu japo visi patikane vyote,nita shukuru kwa maelekezo nitakayo pata.

Kama ukivikosa hivyo vitabu Mkuu naomba nikuazime vyangu hivi :
  1. Kiu
  2. Ijumaa
  3. Risasi
  4. Amani
  5. Sani
Na kwa kukusaidia tu nitakuletea popote utakapokuwepo.
 
Bwana MSA....Mhusika Mkuu wa hadithi zake. Hiki ni kifupi cha majina yake: Mohamed Said Abdulla..
Vitabu vyake ni HAZINA ya elimu. Binafsi falsafa ya "kinyume cha mambo", inayotumiwa na Bwana MSA, IMENISAIDIA sana katika maisha yangu. Huwa naangalia mambo kuanzia upande MWINGINE wa wengine wanavyofikiria. TUKIKUTANA, huwa na mwanga ZAIDI wa jambo husika....
 
Back
Top Bottom