Wapi nitapata mafunzo ya SAP FICO na SAP Procurement modules

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Posts
4,895
Reaction score
7,047
Wadau nahitaji kuboresha utendaji wangu wa kazi kwa kupata mafunzo ya SAP FICO (Financial Accounting and Controlling) na pia SAP Procurement (MM) modules.

Hivyo nauliza kwa wenye uelewa na hizo modules ni wapi kwa Dar es Salaam ninaweza kupata mafunzo (practical) ya hizo modules zote mbili?
 
Wadau bado nahitaji msaada wenu kuhusu hii mada. Natanguliza shukurani zangu kwenu.
 
Ahsante sana mkuu Nyanyadu. Kwa muda huu niko mkoani kwa siku kadhaa ila nikifika Dar moja ya vitu muhimu ni kuwasiliana na wewe. Ubarikiwe sana.
 
Mkuu Nyanyado salama ndugu? Napenda kukutaarifu kuwa nimefanikiwa kupata sehemu ambayo iko convenient zaidi kwangu kwa ajili ya mafunzo haya na tayari nimeanza. Nashukuru sana kwa utayari wako uliokuwa nao katika kunisaidia pale nilipoleta ombi hili hapa.Siku njema za kumalizia mwaka na pia kuukaribisha mwaka mpya.
 
Nisehemu gani
 
Nisehemu gani
Mimi nilipata tu msaada kutoka kwa mtu wangu wa karibu.Hata hivyo kuna taasisi kadhaa kwa Dar ambazo zinatoa mafunzo hayo japo kwa mtu mmoja mmoja inaweza kuwa gharama kubwa.

Jaribu kuwaona jamaa wa Double Click Consulting Ltd walio pale IT Plaza floor ya tatu. Jengo hilo lipo mtaa wa Ohio jirani kabisa na PPF Tower. Wengine wanaotoa mafunzo hayo ya Enterprise Resources Planning (ERP) System (SAP, SAGE n.k) ni Unique Academy walio pale Upanga jirani na shule ya msingi ya Olympio. Hao namba zao za simu ni +255 22 2153 122. Wapo wengine wanaitwa Twenty Third Century Systems lakini sina contacts zao kwa muda huu.

Kuepuka gharama ni vizuri tu ukaongea na mtu wa kutoka sehemu hizo nilizotaja au sehemu nyingine yoyote mradi tu awe na uelewa wa SAP na kuelewana akufundishe pembeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…