Wapi nitapata bajaji kwa mkopo nafuu

Daviie

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2016
Posts
1,292
Reaction score
1,483
Wakuu Habari!..
Tusaidiane connection jamani. Mara kibao nimekuja humu na nyuzi zangu lakini hakuna mafanikio yoyote. Nimekuwa kama mlalamikaji namimi sipendi kuwa mtu wa kulalamika na kulia lia. Mimi ndoto yangu usiku na mchana nimiliki bajaji ili nijipambanie maisha yangu. Hakuna mtu anayejali tena kuhusu mimi... si Baba, si Mama, si Kaka wala Dada. Nilipata shida ya uti wa mgongo (auto immune reaction) nikajikuta Mlemavu. Miaka mitano nimehangaika sasa nipo tu ndani utokaji wangu ni wa shida, nipo mbali uku vijijini sina connection yoyote namimi nataka nitoke nijipambanie maisha yangu na Afya yangu pia. Nimefatilia Mikopo mbalimbali kote mpaka niwe na zaidi ya Mil 2 ndo wanikopeshe hiyo Bajaji. Sina hiyo pesa na hakuna mtu wakunisapoti nipo mimi kama mimi... Hebu anayefahamu chochote humu ndani tujuzane jamani niwapi nitapata mkopo kwa masharti nafuu i mean nipate mkopo bila kianzio maana kiukweli sina chochote.
Simu: 0625656479 (plz call me if you have any information to help)
Note:
Baadhi ya nyuzi zilizopita nimezifuta kwasababu niliandika kutafuta msaada hasa connection lakini siyo kuchangisha mtu mmoja mmoja, badala yake wadau wakaanza kuniambia niweke namba na picha zangu wanichangie pesa. Nikaweka namba na picha kitu ambacho sikupenda kujianika lakini nikaona isiwe kesi kama kweli wadau watanichangia ni vizuri. Mwisho wa siku hakuna mtu hata mmoja aliyenichangia pesa so picha zangu nikawa nimeweka bure. Leo niseme tu sina nia ya kuchangisha mtu mmoja mmoja Lengo langu nipate mkopo mambo ya bure yamejaa fedheha. Hakuna kitu kigumu kama kuomba pesa maana yatakuja maneno mengi mabaya mara tapeli mara sijui nini n.k so kuepuka hayo maneno ya fedheha nimejihami tu mapema , nahitaji sana msaada na ninateseka sana lakini inaumiza sana kuwa ombaomba.
 
Pole mkuu, waungwana walisema tabu misuko suko ndobkuijua dunia
 
Dah! Pole bro....me nakuombea kwa Mungu tu
 
Tatizo wachangiaji wanakuja na masharti magumu, wanataka nijaze picha kibao halafu wanapotea. Inaumiza

nakuelewa sana mkuu!hebu jitahd usikate tamaa..achana na mawazo ya kukata tamaa na ww sio mlemavu kbs..akili ipo safi kila kitu kinawezekana...labda akili ingekuwa na ulemavu.. mie nitakujia pm sina uwezo ila nitakuja pm jion
 
nakuelewa sana mkuu!hebu jitahd usikate tamaa..achana na mawazo ya kukata tamaa na ww sio mlemavu kbs..akili ipo safi kila kitu kinawezekana...labda akili ingekuwa na ulemavu.. mie nitakujia pm sina uwezo ila nitakuja pm jion
Karibu!
 
Mkuu naenda kwa DC ukiwa na vyeti vya hospital kama uthibitisho kwa tatizo lako,kisha mueleze tatizo lako, ukikosa msaada nenda kwa RC,ukikosa jitahidi ufike ikulu kwa JPM,nakushauri hivi sababu nina ushahidi zaidi ya watu wanne wameenda kwa jpm na wote wamepewa bajaj,ila wao ni walemavu wa miguu
 
Thanks umenipa nguvu. Mimi pia miguu ndo shida mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…