talentbrain
JF-Expert Member
- Oct 5, 2009
- 1,187
- 760
Amani kwenu wadau wa biashara.
Ndugu zangu huko kijijini wamefanikiwa kuchimba madini ya ruby kwa walivyo niambia, yanakadiriwa kufikia robo tatu ya KG. Ila hawajui wapi wayauze na pia hawana vibali vya uchimbaji maana kwa uwezo wao hawawezi kuwa nao. Pia natambua utata wa kisheria uliopo juu ya umiliki wa madini. maana kwa sheria ya madini iliyopitishwa miaka michache iliyopita hata ukiokota madini uko kwenye kosa kisheria.
Naomba msaada wenu, ni wapi ndugu zangu hawa wanaweza kuuza madini yao kisheria na walipe kodi huku wakipata stahili zao bila kupunjwa??
Nimepitia mitandaoni na kupata bei za kimataifa na inaonesha madini haya yanathamani si haba.... Ila ni wapi wanapoweza kuuza na wasikutana na matatizo ya kisheria?? ni kipi wafanye??
Naweza kuwa nimechanganya madesa katika uandishi wa hoja yangu.... Nisameheni!! Ila dhamira yangu ni kuwasaidia ndugu zangu hawa wasije uza at black market au wakayauza kwa bei ya hovyo kama wazee wetu wakati wa ukoloni walipobadilisha kwa shanga!!
nategemea majibu yatayonisaidia.
Tuwasiliane kwa taeatibu zaid nitakuelekeza vizuri na watafanikiwa ...ila kwanza ni ruby Gemstones ama ni ya kwenye mwamba karandam kama ile ya mpwapwa...??
Sijaiona!! wanaileta week ijayo. Wameichimba sielewi ni kwenye miamba au kwenye ardhi ya kawaida.....
Rubby ya ukweli inapatikana kwenye maji chini kabisa baada ya kutoboa mwamba ila kama ni makpishoni kapishoni yanapatikana juu juu tu kwenye miamba ya juu. Rubby ni madini ghali sanaa...linawaka vizuri sanaa ukilikuta ndio lenyewe lina rangi ya Big G ama ile taa ya nyuma ya gari ikiwaka usiku ndio namna Ruby inavyokuwa . Madini safi sanaa kupigia biashara.
Kuuza kisheria kwanza kakate leseni ya kufanya biasha ya madini ua ya mchimbaji madini, kisha peleka madini TRA yakakadiriwe dhamani, kisha lipa kodi, sasa unaweza kuuza popote kisheria,
Lakini kama unataka pesa na si sheria, njoo Arusha mabilioni yapo yanasubiria madini ya aina zote.
Kaka ni milioni 300 au umekosea kuandika. Mi navojua carat moja ya ruby ni kama dollar 500. Sasa how comes gram moja imefika mil. 300?Rubby real gem isiyo na sukari wala crack , Gramu 1 ni zaidi ya Mil 300. Kwa hapa Dsm kuna matapeli ya kufa mtu walishamtapeli mpaka Mama Anna Mkapa sio watu kabisa hao ! Soko zuri lipo Arusha au Tanga kuna wa Thailand wanatoa bei nzuri nao
Rubby real gem isiyo na sukari wala crack , Gramu 1 ni zaidi ya Mil 300. Kwa hapa Dsm kuna matapeli ya kufa mtu walishamtapeli mpaka Mama Anna Mkapa sio watu kabisa hao ! Soko zuri lipo Arusha au Tanga kuna wa Thailand wanatoa bei nzuri nao
Kaka ni milioni 300 au umekosea kuandika. Mi navojua carat moja ya ruby ni kama dollar 500. Sasa how comes gram moja imefika mil. 300?
Jamaa huwa ana kamba. Alishawahi kusema "mercury nyekundu" inauzwa billions of shillings, wakati hata aina hiyo ya mercury ni myth tu haijawahi kuwepo.
Akikupa story za rupia na madini yaliyoachwa na Wajerumani utachoka mwenyewe.
I will come to PMmozambique mm nimeuza bei mzuri sana tena hakuna mizengwe.kama unataka msaada tuwasiliane
Soko la uhakika ni Arusha ule mtaa nimeusahau jina lakini ntakuambia later na wanunuzi wazuri ni Wathailand . Kwa upande wa Dsm yupo mmoja wa Australia naye mzuri. Cha muhimu wacha yaje kwanza ili uangalie quality kuanzia hapo hakuna kitakacho haribikaa
Kaka ni milioni 300 au umekosea kuandika. Mi navojua carat moja ya ruby ni kama dollar 500. Sasa how comes gram moja imefika mil. 300?
Muwe makini pia mtakao enda kununua msije pigwa mkaja kulalamika huku jf
Ushauri kwa ambaye atavutiwa katika hilo dili hakikisha una servilance ya kutosha na hata uwe na tails kibao au ma sniper , hii biashara kwetu sisi haina tofauti na zile biashara za ngada.. Point ni kwamba hutakiwi kuamini hata kama utapewa pesa mpaka vyote vi balance.