Wapi naweza kuuza matikiti yangu?

Wapi naweza kuuza matikiti yangu?

yaser

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
1,361
Reaction score
299
Habari zenu wadau hasa wale wenzangu na mimi walioamua kujikwamua kwa kukiendea kilimo.

Baada ya msoto wa muda mrefu niliamua kukiendea kilimo cha matikiti na hapa ninapoandika uzi huu matunda yameshakua tayari kwa kuliwa tatizo limekua soko kwani nimewafata wateja kama watatu naona wananipelekea kutaka kujiona tena sina thamani maana hata gharama zake hazirudi kwa bei wanayonitajia. Nimelima heka mbili maeneo ya KIMBIJI (Kijaka) Dar es salaam ambapo nilipishanisha katika kupanda kwani kwa sasa heka moja iko tayari nyingine bado kama siku 14 yavunwe pia.

Mwenye mawazo anisaidie wadau maana nina headache kali sana yani dah. Kwa mzigo uliopo tayari ni kama tani tatu hivi yapo makubwa sana na size ya kati kwa kifupi yamependeza.
ImageUploadedByJamiiForums1470150811.209523.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1470150830.967992.jpg


Napatikana kwa 0713806766.
 
Habari zenu wadau hasa wale wenzangu na mm walioamua kujikwamua kwa kukiendea kilimo. Baada ya msoto wa muda mrefu nliamua kukiendea kilimo cha matikiti na hapa ninapoandika uzi huu matunda yameshakua tayar kwa kuliwa tatzo limekua soko kwan nmewafata wateja kama watatu naona wananipelekea kutaka kujiona tena sina thaman maana hata gharama zake hazirud kwa bei wanayonitajia. Nmelima heka mbili maeneo ya KIMBIJI (Kijaka) Dar es salaam ambapo nlipishanisha katika kupanda kwan kwa sasa heka moja iko tayari nyingne bado kama siku 14 yavunwe pia. Mwenye mawazo anisaidie wadau maana nna headache kali sana yaan dah. Kwa mzigo uliopo tayari ni kama tani tatu hvi yapo makubwa sana na size ya kati kwa kifupi yamependezaView attachment 374985View attachment 374986
Napatikana kwa 0713806766.
Ule mkutano wa chama chako Dodoma juzi lilikuwa soko zuri sana.
 
Good sana kiongozi. Naona kitu kimekubali haswaaa.

Vipi umeshajaribu kutafuta wateja wa jumla kwenye masoko makubwa kama Temeke-Stereo, Ilala, Kisutu, n.k ?

-Kaveli-
 
Dar mbona soko lipo!! Ongea na madalali wa soko la buguruni, tandika , kariakoo na mabibo soko la ndizi , utafanikiwa, au ndo wamekupa bei ya chini?
 
Mpigie Nape au Ole Sendeka aje anunue ukiwakosa hao peleka Lumumba buku 7 fc watayashambulia yote
 
We tafuta meza masoko tofaut idad ambayo unaweza kuimudu!! Kisha safirisha uuze rejareja na mengine tafuta wafanyabiashara uwazie !! Kuwa name moyo wa uvumilivu utafanikiwa na usiangalie ni lini yataisha...(fight )
 
Kama Una Link Za Nairobi Kenya Hebu Ulizia, Nasikia Huko Ndio Kuna Uhakika Wa Bei, Wanakuja Kuchukua Wao Shambani
 
Kaka Usikate Tamaaa, wala usijipe kichwa Kuuma&Dont ever Mind those who are here to Disappoint you, Cha Msingi vuta Subira Watu wa Masoko watakupa muongozo mwema ni wapi Uanzie kwenye kufanikisha Hilo...Hii ndio Jamii forum we Believe in Here..mambo mengi Yamewezekana through hapa...Just wape Muda kidogo watakuja kukupa mwongozo wapi uanzie..Btw hongera kwa Kukuza, ni hatua Kubwa muhimu..Umeonyesha Jitihada na Ujasirii mkubwa hadi kuyafikisha Mazao hapo yalipo..Hapa paliposalia Mungu ataweka Mkono wake na Milango itafunguka...na Utauzaa tuu..Just be patient Mzee.
 
Kaka nimeshawahi kuona mtu kama wewe aliamua kukodi canter tani 3 akapeleka sokoni kwa madalali au wanaouza sokoni aidha Buguruni au soko la sterio temeke.

Kumbuka kukodi gari hela unatoa baada ya kushusha mzigo. Kawaida madalali watachukua mazuri na wanayotaka na watakupa hela. Hiyo hela ndiyo utakayolipia gari.

Hayo mengine unatest zari mwanannyamala au masoko mengine makubwa.

Yatakayobaki unatafuta kijiwe unayamwaga na unauza wewe mwenyewe.

Lakini fanya utafiti kwa hayo niliyokuambia.
 
Habari zenu wadau hasa wale wenzangu na mimi walioamua kujikwamua kwa kukiendea kilimo.

Baada ya msoto wa muda mrefu niliamua kukiendea kilimo cha matikiti na hapa ninapoandika uzi huu matunda yameshakua tayari kwa kuliwa tatizo limekua soko kwani nimewafata wateja kama watatu naona wananipelekea kutaka kujiona tena sina thamani maana hata gharama zake hazirudi kwa bei wanayonitajia. Nimelima heka mbili maeneo ya KIMBIJI (Kijaka) Dar es salaam ambapo nilipishanisha katika kupanda kwani kwa sasa heka moja iko tayari nyingine bado kama siku 14 yavunwe pia.

Mwenye mawazo anisaidie wadau maana nina headache kali sana yani dah. Kwa mzigo uliopo tayari ni kama tani tatu hivi yapo makubwa sana na size ya kati kwa kifupi yamependeza.View attachment 374985View attachment 374986

Napatikana kwa 0713806766.
Ningeweza kukusaidia kutafuta soko...
Ila baada ya kugundua kuwa walioko kwenye AVATAR yako wamesababisha niisome NAMBA mara kadhaa siwezi kukusaidia tena...
Kwani mpaka sasa bado naendelea kuisoma tarakimu ya kirumi taratibu..!
 
Ningeweza kukusaidia kutafuta soko...
Ila baada ya kugundua kuwa walioko kwenye AVATAR yako wamesababisha niisome NAMBA mara kadhaa siwezi kukusaidia tena...
Kwani mpaka sasa bado naendelea kuisoma tarakimu ya kirumi taratibu..!


Hahahaaa mkuu nimeipenda hii... akawauzie CCM eeh?

JF raha sana.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom