Wapi hadhi ya wanawake na ushujaa wa kiume?

mathcom

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,396
518
Habari za siku nyingi wana JF,

Nimekua nje ya hadhira kwa siku nyingi hadi nimehofia kutumbukizwa katika orodha ya R.I.P. members. Baada ya salamu hizo napenda niwakilishe ninachokiona katika jamii zetu zinazo tuzunguka kwakweli hadhi ya wanawake inashuka.

Hapo nyuma kidogo kwa sie ambao umri umeenda tunaweza kukumbuka jinsi ambavyo ilikua vigumu kumpata mwanamke ili ufanye nae mapenzi, hata kama na yeye anakutaka, hata kama alikua ana shida ya pesa au kitu kingine.

Ilikua ni lazime utumie mbinu za kisayansi na ubunifu wa hali ya juu, nadhani hili pia lilichangia kuwapata wasanii nguli na wataalam wa lugha pia!

Leo hii wanawake wamekua kama vocha jamani. Hautakiwi hata ujue kutongoza. Hii inapelekea tuwaone wanawake kama bidhaa rahisi isiyo na thamani. Umahiri wetu wanaume nao umepotea. Hivi leo kweli mwanaume utajisifu umetembea na fulani wakati mwenzio tena wa hali ya chini ametembea na fulani.

Kwaleo naishia hapo kwa swali moja tu

Kipi kifanyike katika jamii kurudisha hadhi ya mwanamke iliyopotea?

Nawasilisha
 
Kuirudisha ile hali itakua ngumu mkuu!!! Maadili yamemomonyoka, ni kuomba tu Mungu na kuongeza jitihada ili yasimomonyoke zaidi.
Wanawake tumejidharau na kujirahisisha sana!!! Imefikia hatua msichana akisema yeye bado hajatumika mbele ya wasichana wenzake anasimangwa na kuchekwa. Ufuska tumeuona ndo fasheni. Inatia huruma sana.
Binti ukijithamini na kushika nafasi yako vizuri mwanaume atakueshimu na kukuthamini pia! Sasa wewe ukiishi kama kiburudisho ndo utakua hivyo.
 
Bora kama umeliona hilo Paprika.. Maombi na juhudi zinatakiwa
Good comments, thanks!
 
Back
Top Bottom