Wapenzi wa Africa Rally Championship (ARC) yupi ni dereva wako bora?

KingPower

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
1,099
1,747
Habari za weekend wakuu!

Nimekuwa mfatiliaji Sana wa kipindi cha Azam sport 3 cha rally kwa takribani miaka 3,

Pamoja na yote mimi kuna madereva nao wakubali Sana kwa Tanzania Mimi ni shabiki wa TUFAIL TUFAIL, ingawa gari Hana,

Tukija kwenye ARC ni mpenzi mkubwa wa Karan Patel, nisema ukweli sijawahi kuona dereva mwenye pace kubwa kama Patel setting ya gari yake ni hatari,!

Ingawa Mwaka jana alikuwa nafasi ya pili nyuma ya Leroy Gomes hawa wote wanatumia Ford Fiesta R5,

Wapo pia madereva wanao Fanya vizur kama akina Yasin Nasser naye ana Ford, Jas Mangat ana Hyundai I 20 R5.

Mwaka huu kwenye kuwania ubigwa wa Africa kuna vita kubwa kati ya Leroy Gomes na Karan Patel

Kuna dereva wa Kenya anaitwa Carl flash Tundo sijui kama nimepatia, huyu jamaa sijui yuko wapi kwenye ARC ni moto wa kuotea mbali pamoja na yule msouth Africa anatumia Toyota, Hawa nadhani wangekuwepo ingekuwa msisimko mkubwa Sana,.

Lakini kwenye huu mchezo kwa Tanzania naona bado tupo nyuma kidogo maana hatuna hata R5 moja ya kubattle kwenye ARC.

Karibu kwa wapenzi wa huu mchezo Tujadili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom