Wapenda Valentine's day someni hapa

maneno roberts

Senior Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
124
Reaction score
38
UKIONA UMEJIANDAA SANA NA VALENTINE UHUSIANO WAKO UNA UFA:

Taratibu tutaelewana tu..Unasubiria Ijumaa ya Tarehe 14 kwa nguvu sana ILI IWEJE?

Labda kama ni Anniversary ya penzi lenu(mlikutana siku ya tarehe hiyo),kwamba ni muhimu kuadhimisha.Wewe penzi lako na mchuchu mmeanza June 12,Valentine inawahusu nini??Mwaka mzima ulikuwa wapi?

Watu wenye Mapenzi STRONG siku hii ni Ijumaa ya kawaida kabisa na wataenda SKYLIGHT tu Thai Village kama hamna kinachoendelea,ila WEWE na uhusiano wako wa Bagia na Chumvi ndo unataka Ufufukie Ijumaa..Halafu Jumapili Mzike tena mpaka mwakani.

Kwangu mimi Valentine ni kila siku,

Nikikuta nguo nzuri ya beby nanunua nampelekea,hata kama ni November 19.

Nikimmiss namfuata ghetto tunaenda Dinner Capetown Fish Market kula.

Akiona kiatu kizuri ananunua anani-surprise,hata kama ni August 7

Penzi lililokufa halitabustiwa na Valentine Day kamwe.

Kama hupendwi hupendwi tu,Penzi halifufuki Ijumaa.

Penzi lililojengwa kwenye misingi Imara huenjoy Valentine kila siku,

Narudia tena,Ukiona umepania sana Ijumaa ujue Penzi lako lina shida kwa sababu hata LEO inaweza kuwa Valentine yako ukiamua.Penzi la kweli halina tarehe kama Kalenda.
 
Reactions: Luv
Wabongo wanatamani ata leo prezdaa angetangaza siku ya mapumziko
 
Na liredio lao la kipumbavu clouds lilivyoshikia Bango ukiwa mgeni utajuwa leo ndio Christmas.
 
Na liredio lao la kipumbavu clouds lilivyoshikia Bango ukiwa mgeni utajuwa leo ndio Christmas.

​



Historia ya Valentines Day - Kanisa na Utawala wa Dola ya Warumi

Siku ya Valentines Day asili yake ni kutoka Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memoria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi sababu ya kutetea waumini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu. Lakini sikukuu hiyo imeenea sana katika nchi za magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya ulimwengu kuisherehekea kama siku yamapenzi kinyume cha dhamira ya Mt. Valentine.

Watawala wa dola ya kirumi walikuwa na fikra za kueneza dola ya kirumi duniani kote na hivyo vijana hawakutakiwa kuoa, ili wawe huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi. Wakioa hawangekuwa na uhuru wa kwenda vitani bali kuwa na famiia zao. Vijana wengi wakawa na mtindo wa kuwa na vimada tu kitu ambacho kanisa lilikukwa linapinga.

Padre Valentine ambaye alikuwa Roma akawa anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa kwani ni dhambi na kitu kisichokubalika mbele ya Mungu. Akawa anafungisha ndoa kwa siri kwenye makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu wachache), alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka amri ya wakuu wa dola ya kirumi.

Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, hivyo Padre Valentin alishikwa na dola ya Warumi na kuuawa kama shahidi mfia dini kwa ajili ya kutetea waamini wake wafunge ndoa badala ya maisha ya ngono zembe bila ndoa.

Wakristo wakawa siku ya kumkumbuka Padre Valentin kama mfia dini sababu ya kutetea maisha ya wanakanisa kuwa wanandoa. Ikaenea katika kanisa nchi za magharibi na hata duniani ambako wanakanisa wanamkumbuka Mt. Padre Valentin. Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na imani ya kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mt. Valentin kama mteteze wa Ndoa.

Maudhui ya siku hiyo kwa wasiowanakanisa imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa bali mradi wanapendana, kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya mfia dini Mt. Padre Valentin aliyetaka vijana wafunge ndoa badala ya kuwa na hawara tu (vimada).
 

Attachments

  • download (3).jpg
    9.8 KB · Views: 358
  • download (2).jpg
    8.8 KB · Views: 366
  • download.jpg
    13.6 KB · Views: 358
habari ndo hiyo
 

Attachments

  • 1392352009360.jpg
    37.6 KB · Views: 146
Hivi divyo inavyotakiwa jamani watu wafunge ndoa na kuacha dhambi,ngono kabla ndoa ni laana(adhabu yake ndogo ni ukimwi) na ngono katika ndoa ni Baraka.Jamani tusipotoshe maana tubadilike!
 
mimi mwenyewe leo nina promise ya siri na mke wa mshikaji!
 
Candid Scope umenimix kabisa,nilichopania kufanya leo mbona kiko opposite na utakatifu!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…