Wapelelezi 4 wa Korea Kaskazini wahusishwa na kifo cha Kim Jong nam

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_94872244_4nksuspects.jpg

Kitengo cha ujasusi nchini Korea Kusini kinaamini kwamba washukiwa wanne wa Korea Kaskazini wanaohusishwa na kifo cha Kim Jong nam ni wapelelezi.

Ndugu huyo wa kambo wa rais wa Korea Kaskazini aliwekewa sumu katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur kulingana na maafisa wa polisi wa Malaysia.

Wanne kati ya washukiwa saba waliotajwa na serikali ya Malaysia wanafanya kazi katika wizara ya usalama ,na ujasusi kulingana na wabunge mjini Seoul.

Haijulikani ni akina nani kati yao wanaotafutwa na serikali ya Malaysia.

Bwana Kim alifariki wiki mbili baada ya wanawake wawili kumfuata katika uwanja huo wa ndege.
Wanasema walidhani walikuwa wanahusishwa kufanya filamu ya mzaha.

Bwana Kim alipakwa sumu kali ya kuua neva kwa jina VX na kufariki akiwa na uchungu mkali kati ya dakika 15-20, alisema waziri wa afya wa Malaysia siku ya Jumapili.

Maafisa wa polisi wa Malaysia walimkamata raia mmoja wa Korea Kaskazini kwa jina Ri Jong Chol siku chache baada ya mauaji hayo.

Watu wengine 6 kutoka Korea Kaskazini wametajwa kuwa washukiwa na wanasakwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Korea kusini ndo wasemaji? Kwa nini chi inayoendelea na uchunguzi hawajaongolea?.
Ndo maana trump anawakazia haya mashirika ya habari kwa kuyaita "FAKE NEWS";
 
Hao Korea kusini sio wa kuwaamini

Sijasema North korea hawahusiki moja kwa moja ila hao Korea kusini waongo sana na wana propaganda sana kuwachafua mahasimu zao walishawahi kusema Kim alimuua waziri aliyesinzia na anti craft lakini hakuna uthibitisho wowote ule ,waongo sana

Siku Kim jong nam anakufa airport walitoa ripoti kuwa alichomwa na sindano yenye sumu na wakawa wanaeleza namna alivyouliwa na wahusika waliomchoma sindano ,swali la kujiuliza tukio limefanyika airport nchini Malaysia wao walijuaje na maofisa wa Malaysia hawakutoa ripoti??

Lakini maofisa wa Malaysia walivyofanya uchunguzi wakatoa ripoti kuwa hakuchomwa sindano Bali prank tu ambayo mwanadada wa miaka 25 raia wa Vietnam alimnyunyuzia Kim jong nam sumu bila kujua ,Korea kusini wakaaibika na uongo wao

Hii habari ni ya kupuuza hawa Korea kusini kila siku wanakuja na propaganda mpya..ni mjinga pekee atayewaamini

Hapa tusubiri ripoti ya maofisa wa Malaysia tu hawa Korea kusini tumeshawazoea na propaganda zao nyingi
 
Sasa kama umeona ni uongo kwa nini umeileta hapa? Kwanza inatusaidia nini sisi?
 
Back
Top Bottom