Malkia amefariki! Tumtakie Mfalme umri mrefu!
Ndivyo Waingereza wanavyosema hivi sasa. Na ni kauli mbiyu ya zamani hiyo.
Ukitazama, utaona kuna mshikamano mkubwa hapa, na mapenzi makubwa yanayodhhirishwa kwa marehemu Malkia Elizabeth.Watu hupanga safu kwa saa hadi 16 tena chini ya baridi kali iliyoanza, wakitembea taratibu kuelekea kutoa heshima za mwisho. Vyombo vya habari saa 24 vinaelezea mambo mazuri yote aliyoyafanya marehemu, na watu wanajitokeza kuzungumzia walivyopokea hisani za Malkia nk.
Na hii.....ndiyo tofauti kati yetu na wao!
Wazungu, hata kama wana tofauti kali na kiongozi wao, akishafariki tu, hukumbuka mazuri yake na kujiepusha kufukua mabaya yake.
Tena, hata katika uhai wa kiongozi, tofauti zozote hata zikiwa kubwa namna gani, zinaelezewa kwa staha kubwa na kuchunga heshima ya kiongozi. Hata kama amewakasirisha kupita kiasi, haitatokea wakamvunjia heshima kwa maneno ya ufidhuli na matusi. Wasingependa hata kidogo familia na watoto wa kiongozi wasikie ufedhuli.
Sasa walinganishe na siye!
Jana, hapa kwenye Jamii Forum kuna jitu liliandika matusi ya kukejeli hata 'akili' ya rais wetu! Usishangae jitu lenyewe likawa ndiyo kwanza limeingia kutoka kwenye shamba lake la tumbaku kule Songea, halijui chochote juu ya uongozi, sembuse mahusiano ya kimataifa......lakini lina 'uhuru' na ujasiri wa kumtukana kiongozi!
Fanya hivyo hapa kama hutaona cha mtema kuni!
Kuna sintofahamu kubwa kwa Waafrika jinsi wanavyoufahamu 'uhuru'.
Ndiyo maana inakuwa vigumu kuendelea. Moja ya sababu ni raia wasio na nidhamu, siku zote hawaoni mazuri na kumpa nguvu kiongozi, watovu wa shukrani, wenye tabia chafu.
Malkia Elizabeth hakufanya mazuri matupu. Kuna sehemu nyingi amekosea kama binadamu....lakini raia wake wakumbuka fadhila na wanamshukuru kwa kuwatumikia.