Wantazania tuwe na matumaini

Wantazania tuwe na matumaini

chawade

Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
21
Reaction score
3
CHAMA CHA WANANCHI NA DEMOKRASIA
CHAWADE
Phone: +255 789113534, +255 715 039991
Mw/Chai – Matombo na Gombero (house No 28)
chamachawade@yahoo.com


Ndugu wanachama wa CHAWADE, napenda kuchukuwa fursa hii adimu kwa heshima kubwa kuzungumza nanyi kupitia WARAKA huu, mambo muhimu juu ya maendeleo ya chama chetu kitukufu CHAWADE.

Jambo la kwanza ambalo napenda kuzungumza nanyi ni hili la maendeleo ya taratibu za usajiri wa chama chetu. Hadi sasa, taratibu zote zinaendelea vizuri juu ya USAJIRI WA KUDUMU hata hivyo kuna changamoto kadhaa ambazo natumaini tutaweza kuzikabili na hatimaye kupata usajiri wa KUDUMU.

Matarajio yetu ni kuwa kama hapatakuwa na mizengwe kwenye tarehe 20/06/2015 tunaweza kuwa tumepata usajiri wa KUDUMU.

Ndugu wanachama, jambo la pili ambalo napenda kuwafahamisha ni juu ya idadi ya wanachama hadi sasa. Kwa juhudi kubwa ambazo viongozi wa chama chetu wamekuwa wakizifanya juu ya kupata wanachama wapya, hadi sasa ninapowaandikia waraka huu, chama chetu kimefikisha wanachama elfu nane na thelathini na tatu (8,033).

Ndugu wanachama, jambo la tatu ambalo napenda kuwafahamisha ni juu ya ushiriki wetu kwenye UCHAGUZI wa mwaka 2015. Katika uchaguzi wa mwaka huu napenda kuwajulisha kuwa tutashiriki kikamilifu kwa kuweka wagombea kwa nafasi za ngazi mbali mbali (URAIS, UBUNGE NA UDIWANI) katika maeneo yote ndani ya nchi yetu.

Ndugu wanachama, endapo itatokea chama chetu kikawa bado hakijapata usajiri wa kudumu hadi kipindi cha uchaguzi, uongozi wa chama chetu utatoa TAMKO juu ya chama gani na wagembea wepi CHAWADE itawaunga mkono kwa mantiki hiyo tuwe na subira muda ukifika tutafahamishana.

Kwa kumalizia, ndugu wanachama, napenda kuwaomba kuendelea kuwa na SUBIRA pamoja na uvumilivu maana chama chetu bado kipo kwenye mchakato wa kupambana na kuhakikisha tunapata usajiri wa KUDUMU.

Nawashukuru sana kwa ushirkikano wenu katika kukijenga chama chetu.

Asanteni sana na Mungu awabariki.


CHAWADE!!! KWA PAMOJA TUTASHINDA!!!


Shabiri Mpaka
Mwenyekiti Chawade Taifa.
 
Wantazania ndo wakina nan wanaishi nchi gan?
Ulimaanisha Watangaza nia au Watanzania?
Ue una "edit' kazi yako mkuu
 
Ka hiyo ndo mlivyotumwa na nepi? Huoni kama jina la kikundi chenu linafanana kabisa na chama dume CHADEMA. Mwambieni huyo mwehu wa lumumba hizo ni propaganda za zamani sana
 
Mimi sio mwanachama! Hata hivyo, naona kama kuna miweweseko ya CCM hapa!
 
Back
Top Bottom