MCHUNGAJI alikuwa anawaombea waumini wake akauliza;
MCHUNGAJI: Wangapi wanataka kuokoka inueni mikono niwaombee.....hakuna aliyeinua mkono. Tajiri mmoja akapita mbele na kupanda madhabauni na kutangaza
Tajiri: Jamani mchungaji anasema wanaotaka kuokoka wanyanyue mikono juu jamani.....mtoto mmoja peke yake akanyanyua mkono, tajiri akatoa laki tatu mfukoni akampa yule mtoto.
Tajiri: Haya jamani ninaomba nirudie tena niwaombe wanaotaka kuokoka wanyooshe mikono juu ili Mchungaji atuombee.....watu wote wakanyanyua mikono juu, tajiri akamgeukia Mchungaji ili awaombee akakuta na mchungaji nae kanyanyua mkono juu...