Habari za mihangaiko wana JF,
Leo nimekaa na kuwaza jinsi wana dada wanavyotusumbua pindi tunapokua kwenye mizunguko yetu ya kila siku.
Wangapi walishakutana na hiki kituko? Unakuta upo zako kwa ndugu jamaa na marafiki unapiga stori mbili tatu huku mkifurahia maisha yanavyosonga.
Ghafla mke/msichana wako anakupigia simu na kukwambia baby njoo tena mimi naogopa kukaa peke yangu, unaenda.
Siku inatokea mnagombana anatoka kama saa saba za usiku eti hataki kulala ndani. Haya ni maigizo tuwe makini, kwenye nyumba anaogopa ila nje tena usiku mkubwa haogopi anatoka zake.
Sasa ndo wanaume wenzangu mkae mkijua kwamba siku akikwambia tena anaogopa mwambie azime taa alale maana si kwa sanaa hiyo.