Wanawake wanaongoza kudai talaka katika ndoa

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,536
“Nipe talaka yangu, nataka tuachane”. Ni maneno rahisi kutoka kwa mwanamke kuliko mwanamume, tafiti zimebainisha.

Utafiti uliofanywa na mwandishi wa Michael Rosenfeld unaonyesha kuwa kwa asilimia 70 wanawake huwa chanzo cha talaka kwa kuidai pale uhusiano unapokwenda kombo. Rosenfeld aliwahoji wanawake 2,000 waliopewa talaka na kugundua kuwa 1,400 walizidai wenyewe.

Kwa nini wanadai talaka?

Furaha,amani na upendo ni vitu vinavyochangia kwa kiasi kikubwa ndoa kustawi na familia kuwa bora. Kinyume na hapo maisha ya ndoa yanaweza kuwa machungu kiasi cha wanandoa kufikia uamuzi wa kutengana.

Inapofikia hatua hiyo suala la talaka linachukua nafasi hapo ndipo ugumu unapoanza kutokea hasa kwa wanawake.

Mwanasheria wa Afrika Kusini aliyebobea katika masuala ya talaka, Cynthia Rhoades anasema kipindi cha kudai talaka humuia vigumu mwanandoa yeyote.

Hata kama itatokea wewe ndiye unataka talaka lazima kuna ugumu fulani utapitia katika maisha kukabiliana na uamuzi huo.

Kwa mujibu wa Rhoades, kuna mambo kadhaa ambayo mtu unapaswa kuzingatia na kuyafahamu kabla ya kudai talaka.

Siyo lazima mahakamani

Unaweza kupata wakati mgumu hasa pale unapofikiria suala la talaka, litakulazimu kuingia mahakamani.

Hiyo siyo kweli mnaweza kufuata hatua zote za kupata talaka bila kufikishana kwenye chombo hicho kikubwa cha sheria.

Hilo litawezekana endapo wote kwa pamoja mtaridhia uamuzi wa kuachana na mtashirikiana kuhakikisha lengo lenu linatimia.

Utahitaji msaada

Kwa mujibu wa Rhoades, mchakato wa kupata talaka unaweza kusababisha msongo wa mawazo na wakati mwingine kutia hasira. Unapaswa kuweka akilini kuwa kwa hali hiyo lazima utahitaji msaada kutoka kwa watu wengine. Hapo ndipo mchango wa marafiki na ndugu unapohitajika.

Masuala mengi ya kisheria yanaweza kuwa mageni kwako hivyo utahitaji mtaalamu ambaye anaweza kukusaidia ili kichwa chako kisivurugike zaidi.

Gharama zitahitajika

Unapofikia uamuzi wa kufungua kesi ya kudai talaka unapaswa kutambua kuwa kuna gharama utakabiliana nazo.

Hapa utatakiwa kumlipa mwanasheria sambamba gharama unazoweza kukutana nazo katika maisha mapya unayokwenda kuyaanza. Inashauriwa kupunguza matumizi katika kipindi hiki huku ukijiweka mbali na madeni yasiyo na umuhimu.

Inaweza kukuchanganya

Unapaswa kutambua kuwa mchakato mzima wa kupata talaka unaweza kukuchanganya ndiyo maana inashauriwa kumtafuta mtu aliyebobea kwenye sheria ili aweze kukusaidia.

Mtu huyo ndiyo atakuwa wa wajibu wa kukuelezea vifungu vyote vya kisheria ili uweze kupitia mchakato huo bila kupata ugumu.

Fikiria kabla ya kuamua

Katika kipindi hiki unatakiwa kutoa maamuzi mengi ya muhimu. Kabla ya kufanya hivyo jaribu kufikiri kwa kina ili kujiridhisha kuliko kukimbia kutoa uamuzi. Ni vyema ukapata ushauri na maelezo kwa kina kutoka kwa watu wako wa karibu juu ya suala unalokwenda kulitolea uamuzi.

Mwanasheria ambaye pia ni Wakili wa kujitegemea kutoka Kampuni ya Moriah Law Chambers, Justine Kaleb anasema ndoa ni makubaliano ya halali baina ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja. Anasema ndoa zinapotaka kuvunjwa huwa katika makundi mawili yaani ndoa batili na batilifu. Anafafanua kuwa ndoa batili ni ile ambayo wanandoa walikuwa wanaishi bila kukubaliana kisheria yaani hawakufunga ndoa ya kidini wala ile ya Serikali.

“Ndoa batili inapotaka kuvunjwa hufikishwa mahakamani kuthibitisha tu kwamba haikuwa ndoa halali, hivyo haiwezi kuendelea kuwapo, hii mara nyingi inaweza kuwa mwanamume au mwanamke alikuwa chini ya umri wa miaka 18, alishafunga ndoa awali, uhusiano wa kindugu kwa wanandoa au mmoja kati yao hakuwa na hiari na ndoa husika,” anasema Kabel.

Anasema ndoa batilifu ni ndoa ambayo ilifungwa kisheria, lakini wanandoa wanataka kuivunja kwa talaka nayo ina vipengele vingi vya kuzingatiwa.

Anasema kabla ya wanandoa hao kuivunja kuna taratibu ambazo wanapaswa kuzifuata kabla ya kufika mahakamani kwa ajili ya kuvunja ndoa yao.

Kabel anasema jambo la kwanza kwa wanandoa wanapaswa kufika katika baraza la usuluhishi wa ndoa, baraza lina uwezo wa kusuluhisha na iwapo ikishindikana ndipo watapaswa kwenda mahakamani kwa kibali maalum.


“Baraza litatoa kibali kwa wanandoa kupeleka shauri la talaka mahakamani, lakini sababu lazima zielezwe wazi na vidhibiti vitolewe maana wengine hutunga makosa,” anasema Kabel.

Chanzo: Mwananchi
 
Tatizo viburi vimetawala kujiona wako sawa na wanaume kisa wanamiliki gari, kiwanja na asset zingine zinawapa viburi sana hizi na baadhi yao utakuta wamehongwa au kuvipata kwa nia isiyo halali
 
Back
Top Bottom