Mimi Mphamvu Letsholonyane, naamini kuwa hao waliodai hayo ni kikundi kidogo cha wanawake(na inawezekana wanalipwa) kinachosemea mioyo ya wanawake wote wa Songea. Nakiri kuwa na mashaka na uwezo wao wa kufikiri, badala ya kuangalia vitu vya msingi kwenye huo unaoitwa uchochezi, wanaangalia kaka mkubwa anasema nini kuhusu hayo. Nahisi siku Kikwete akitamka wanaCCM wote ni mataahira, wao wataunga mkono kwa kauli moja, na atakayepinga atakuwa mchochezi na asiyekitakia mema chama!