Wanawake tunawaheshimu sana

DOGofGOD

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
1,341
Reaction score
480
Amani ya bwana itawale jamvini,

Hii tabia yetu ya baazi sisi wanaume kuwaletea makuzi mademu zetu na wake zetu itatutokea tu puani ipo siku.Mambo ya kumrudia mkeo usiku, dharua, vipigo, manyanyaso, lundo la michepuko n.k.

Sio sifa ila ni sawa na kucheza na mdomo wa simba mweny njaa. Fanya ako mfanyie yote lakini ukae mkao wa kula.Siku atakapochoka hizo drama zako ujue imekula kwako huu ni ushauri tu wa bure kwako.Unataka uzingatie hutaki shauri yako.

Boya mmoja nchini naigeria si kamletea makuzi mkewe.Ebu uliza kilichompata? Mkewe kamchanganyia mchuzi wa sumu ya panya kwenye rosti la maini. Ebu uliza tena nini kilitokea? Huyu boya kwasasa tunavyoongea hatunae tena.

Hawa wanawake tuwaoneni hivi hivi tu na wanja zao.Ila Inabidi tuishi nao kwa akili sana. Kwasababu wanatembea na roho zetu mkononi.Tunapashwa tuwaheshimu sana tuache makuzi. Wanauwezo wa kutufanya chochote wanachotaka wakati wowote hii skendo ya naigeria imenifanya niwe mpole sana.

Shikamooni wanawake manake dah mnatisha sana
 
Ki ukwel!
Wanawake tuna roho nzur mno ila upande wa pili ni hatar mfano hakuna mfano
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…