Wanawake Shtukeni! Sera za haki sawa chanzo cha kuvuruga ndoa zenu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Zamani kabla huu udwanzi wa haki sawa, ndoa zilikuwa zinadumu sana. Lakini baada ya kuleta haki sawa tu ndoa siku hizi ni miezi mili ishavunjika. Wanaanza kulala mzungu wa pili, kila mtu anajitegemea kama bachela na hata salamu hawapeani. Haya mambo ya haki sawa yaishie hukohuko Serikalini sio kwenye ndoa zetu.

Ukitaka ndoa yako idumu, achana na hawa watetea haki za wanawake. Kwani sisi wanaume ni wanyama hadi mtuundie NGOs?

Wewe unayetaka kuolewa au uliyepo kwenye ndoa, Mheshimu naMsikilize mume wako, Mfundishe, mshauri hata kumuelekeza.

Eti wanawake wa siku hizi wanafurahia kuona mume wake akiosha vyombo baada ya kula, akideki, akifagia, akipika na kubembeleza mtoto alale.

Wanawake wa siku hizi wanafurahi wakiona waume zao wakitangulia nyumbani saa 12 jioni huku mwanamke akija saa tano Usiku.

Wanafurahi kuona anaporudi kwa kuchelewa haulizwi alikuwa wapi, hataki kuona mwaume akigusa simu yake, hataki kupangiwa cha kufanya na mume wake.

Wanawake wa siku hizi wanapenda kuona waume zao wakitandika Vitanda na kuchomekea chandarua ikiwemo kupelekewa maji bafuni. Eti Mwanaume kama unashindwa kufanya hayo, tafuta mdada wa kazi afanye.

Hawa haki sana Wanawadanganya sana. Nia yao wanataka baadae waje wawasimiame katika kugawana vitu baada ya kutandikwa talaka na masikio yake.

Mfano mimi ili unifanyishe hizo kazi, nipe limbwata kwanza. Vingenevyo utaambulia patupu.

Naamini huo sio mpango wa Mungu kunitafutia msaidizi wa kunikalia kichwani. Manaake wanawake wa siku hizi wanajifanya wao ndo kichwa cha nyumba kisa tu Mumefunga ndoa kanisani. Kudadadeki...
 
Mimi sishabikii usawa kati ya mwanamke na mwanaume, tunaoamini katika uumbaji mwanaume aliumbwa mwanzo kisha akapewa msaidizi ambaye ni mwanamke anayetokana na yeye, so mwanaume atabaki kuwa top na mke awe chini yake no matter what, ila usaidizi huo usitafsiriwe kuwa ni utumwa, basi mke afanyishwe kazi kama punda kisa msaidizi,Mwanamke afanye kazi nyepesi zilizo ndani ya uwezo wa maumbile yake. Mume kumsaidia mke majukumu ya nyumbani sio ubushoke, ni katika kujali na kuonyesha mapenzi kwa mke. Kwa sababu mke naye anachoka.
 
Ni kweli wameibuka watetezi wengi sana wa kina mama hadi wamepitiliza ni mke wako kabisa lakini unaambiwa thubutu kumsukuma kwa bahati mbaya then upelekwe kwenye dawati la jinsia na watoto huna bahati...
Lakini pia kuna wanaume wakatili jamani, mke anapigwa mpaka anaharibiwa sura, kuna baadhi ya jamii mwanamke hana thamani, kwa kiasi fulani hizi harakati zimewasaidia japo wengine wanazitumia vibaya kubaka mamlaka ya wanaume ndani ya ndoa..
 
Kuna wanaume wanyanyasaji sana aise.....unafikiri hao watetezi au dawati la jinsia ndio linawapa kiburi wanawake? Au utandawazi na wanawake kuwa na elimu na pia kujitambua zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali
 
Kuna wanaume wakatili ni kweli kabisa ila nahisi utetezi huu kwa wanawake umepitiliza mno hadi mtu unaishi na mke wako kwa hofu na mashaka hata ukimkanyanga kidogo tu anakuambia niende kwenye dawati...na imepelekea hadi unasikia sasa wanaume hadi kupigwa na wanawake ndani ya nyumba wanapigwa...Imefika mahali na wanaume tuungane tuunde chama chetu cha kututetea sasa...
 
Pamoja na Elimu ila kuna misukumo mingi sana inayowafanya wanawake wengine kuharibika mfano..Women Empowerment, Gender Equality sijui Women rights....ukijumlisha yote hivyo na ukiangalia kwa undani wake mambo yanayozungumziwa huko dhidi ya wanaume na haki za wanawake...Kwa jamii zetu za kiafrica na mila zetu ngumu sana kuwa applicable....
 
Kuna wanaume wakatili ni kweli kabisa ila nahisi utetezi huu kwa wanawake umepitiliza mno hadi mtu unaishi na mke wako kwa hofu na mashaka hata ukimkanyanga kidogo tu anakuambia niende kwenye dawati...na imepelekea hadi unasikia sasa wanaume hadi kupigwa na wanawake ndani ya nyumba wanapigwa...Imefika mahali na wanaume tuungane tuunde chama chetu cha kututetea sasa...
Teh teh teh, naamini hizo case za wanaume kupigwa ni chache sana ukilinganisha na za wanawake, au pengine ni kwa vile mwanaume kupigwa "ni siri ya ndani" but ukiona umemkanyaga mke au kumpush kwa bahati mbaya akatishia kukushtaki basi ujue ni ndoa iliyoshikiliwa kwa uzi wa buibui...
 
Mimi sishabikii usawa kati ya mwanamke na mwanaume, tunaoamini katika uumbaji mwanaume aliumbwa mwanzo kisha akapewa msaidizi ambaye ni mwanamke anayetokana na yeye, so mwanaume atabaki kuwa top na mke awe chini yake no matter what, ila usaidizi huo usitafsiriwe kuwa ni utumwa, basi mke afanyishwe kazi kama punda kisa msaidizi,Mwanamke afanye kazi nyepesi zilizo ndani ya uwezo wa maumbile yake. Mume kumsaidia mke majukumu ya nyumbani sio ubushoke, ni katika kujali na kuonyesha mapenzi kwa mke. Kwa sababu mke naye anachoka.
Safi sana mtaani. Umenena ukweli...
 
Back
Top Bottom