Wanawake na Urais Tanzania

Wanawake na Urais Tanzania

Birds in bush

Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
42
Reaction score
23
Naanzisha hii thread ili tupate maoni kati ya wanawake ambao wanaweza kuwa viongozi wa nchi kati ya Rose Migiro, Anna Makinda na Prof Tibaijuka. Je Rose Migiro anaweza kuwa Rais wa Tanzania hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa naibu katibu mkuu wa UN pamoja na kwamba hakupewa nafasi ya kumaliza ngwe yake ya pili kwa sababu ambazo hazijulikani!!!! Pili Anna Makinda ambaye ameliongoza bunge la JMT kwa kipindi cha takribani miaka minne sasa huku kukiwa na kelele nchi nzima namna anavyoongoza bunge hilo na Prof Tibaijuka, mama wa shoka ambaye alikuwa UN habitat ambapo baadaye amekuwa Waziri wa ardhi licha ya kuendelea na kuwa na miji isiyopangika katika nchi yetu, ujenzi holela kila sehemu kana kwamba hakuwa hata mtu wa kusema sasa imetosha miji yetu kujengwa hovyo hovyo utadhani uko nchi ambayo wananchi hawajui hata umuhimu wa kujipanga vizuri ili iwe rahisi hata kupata huduma za kujamii.
Leteni mawazo
 
Siku ambayo U.S.A itakapo kuwa na rais mwanamke ndipo nitashauri na sisi tuwe na rais mwanamke.

Tunazaliwa na wanawake na tuna waheshimu kama mama zetu,ila ipo siku hi 50,50 itatuponza wanawake ni wiki kama historia inavyo sema toka enzi na enzi (that is nature).hawa wanawake tunaambiwa kuwa ni icon ya wanawake wengi duniani ni kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa tu.

Jiulize swali dogo,toka umedadisi kuhusu vitu vilivyo gunduliwa duniani vyenye umuhimu mkubwa ni kipi amegundua mwanamke hi inamanisha utofauti mkubwa sana kati ya mwanamke na mwanamme toka kufikiria hadi kimaamuzi
 
Tuanze na wanawake walio katika hili Bunge la JMT au hata waliokuwa katika BMK - ni wangapi ambao wamesimama kidete kumtetea mwanamke mwenzao ambaye ndiye muanga mkubwa wa mfumo huu kandamizi na ufisadi? Wangapi wamewatetea akina mama wanaolala sakafuni katika wadi za kujifungulia za Muhimbili, Temeke, Mwananyamala, na kwingineko? Wanawake vijijini wanateseka sana hawa viongozi wanashindana nanai amevaa wigi zuri la nywele, nani kavaa cheni za dhahabu, nk!!!. Kwa bahati mbaya mwanamke akiisha pata cheo anakuwa fisadi mbaya sana kuliko hata mwanamume. Wakati huo huo hata hawa wanawake wanaolala sakafuni wakati wa kujifungua ndio wanakuwa mstari wa mbele kuipigia kura CCM. Ndiyo, mwanamke ni kiumbe tata sana (wanatuzaa lakini ni watata sana, na hawafai kabisa kushika usukani wa kuongoza jamii hii, tena iliyokwishaoza). Akina mama mtanisamehe - sina jibu la ka nini viumbe wanawake wako hivyo.
 
hakuna mwanamke au mwanaume ndani ya ccm mwenye sifa za kugombea uraisi 2015 wote mafisadi wakubwa hawafai
 
Siku ambayo U.S.A itakapo kuwa na rais mwanamke ndipo nitashauri na sisi tuwe na rais mwanamke.

Tunazaliwa na wanawake na tuna waheshimu kama mama zetu,ila ipo siku hi 50,50 itatuponza wanawake ni wiki kama historia inavyo sema toka enzi na enzi (that is nature).hawa wanawake tunaambiwa kuwa ni icon ya wanawake wengi duniani ni kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa tu.

Jiulize swali dogo,toka umedadisi kuhusu vitu vilivyo gunduliwa duniani vyenye umuhimu mkubwa ni kipi amegundua mwanamke hi inamanisha utofauti mkubwa sana kati ya mwanamke na mwanamme toka kufikiria hadi kimaamuzi

Kwa hiyo unataka kutuambia Afrika yote kuna wanawake hakuna wanaume maana hakuna kitu chochote muhimu duniani alichogundua mwafrika!
 
Mchango wako unaonesha hujui historia ya sayansi na ugunduzi,wanawake walikua hawaruhusiwi kujifunza kusoma na kuandika,walipo pigana wakilishnda hilo,wakawa hawaruhusiw kusomea udactari,walipo limaliza wakawa hawaruhusiwi kupiga kura mpaka baada ya vita ya kwanzaya dunia sababu ndio waliendesha viwanda vya kutendgeneza siraha wakati wanaume wako vitan.Google tafta historia ya wanawake scientist Maria curie ufute uo ujinga wako kabla hujawatukana wanawake walio kuzaa.Shame on you
 
Back
Top Bottom