Hahahah umenikumbusha zamani nilikuwa nina hasira mtu apokee simu sio yake.
Basi bwana mwenye simu na aliyepokea simu majina yanafanana halafu ni ndugu, sasa sauti ya muhusika naifahamu, namwambia namtaka fulani (nataja jina), ananiambia ndio mimi, kila nikisema sio wewe yeye anabisha, "nilishusha mafuriko ya maneno mabaya" hakutegemea nikamwambia kama kakutuma uchezee akili yangu siku nyingine hutarudia.
Duuuh huu ndio ulikuwa mwisho wa kuongea hovyo kwenye simu, maana nikaitwa kutambulishwa yule nilomtukana, nilitambulishwa vizuri utapenda,"kaka fulani huyu ndo fulani mke wangu mtarajiwa"(hapo nyumbani washapeleka posa washapangiwa mahari ndo wanajipanga wapeleke), nae akajibu, "anhaaa, nashukuru kukufahamu, lakini si ndio huyu ulozaa nae" akajibu ndio basi kaka yake akamalizia, "kama ndio huyu nafurahi sana maana nilishasikia sifa zake kabla, anafaa"
Mimi macho chini pale nikaanza tena kuomba samahani, nashukuru alikuwa muelewa akanisamehe na hakuna aliyejua zaidi ya sisi watatu, ila nilijifunza sana siku ile(huyu ndugu yake alikuwa anaishi mbali hivyo sikuwa namfahamu kabla na jina nilishatajiwa ila nilisahau). Sitarudia teeeeenaaaaaaaa