Wanawake mnaumia kwa kiasi gani waume zenu kutoka nyumbani usiku kwenda kuangalia mpira?

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Mimi binafsi nikiri kuwa na mpenzi na shabiki mkubwa wa mpira wa miguu na michezo ya mieleka, kwa wale wanaofatilia mpira wa ulaya kuna mechi za katikati ya wiki huwa zinachezwa usiku sana mara nyingi huanza kama si saa nne na dk 45 basi saa tano kamili usiku.

Nilikuwa lazima niende kwenye mabanda ya video au bar kuangalia kitu ambacho nilijua na kushuhudia kikimkera sana mpenzi wangu japo alikuwa ananiruhusu niende nilikuwa namwona hana furaha nikajionja nikasema huu mpira utakuja kuvunja ndoa yangu.

Nikajichanga changa nikaamua niende kununya DSTV ili niwe naangalia nyumbani mpenz wangu alifurahi mno siku naenda kununua nikakuta kaenda kununu kuku wa kienyeji akasema leo mme wangu ninafuraha sana akatengeneza juice ya embe nikamwona mda wote anafuraha na kukaa karibu yangu.

Nikamwambia kulipia kifurushi kikubwa hicho unaangalia mechi zote ni 184000/= akaniambia we unashilingi ngapi nikamwambia nimebaki na 100000 tu Akaingia ndani akanipa 100000 akaniambia keep change, mke wangu namjua bahili sana siyo kutoa laki haraka haraka ndipo nilipojua nilikuwa namwumiza sana.

Sasa napenda nisaidiwe wanawake mnaumia kwa kiwango gani tunapotoka kwenda kuangalia mpira usiku? Huku mkijua waume zenu ni wanazi wa kutupwa wa mpira.
 
Mimi namruhusu kwa moyo mmoja sababu huo mpira sio kila siku ni mara chache, nikimuambia aangalie nyumbani hawezi anaishia kulala, labda tu kama ni mechi ambayo na mimi nataka niangalie ndiyo atabaki ili tutizame wote.

Ndoa isiwe sababu ya kukoseshana furaha zingine, wanawake wengi wanahisi labda mwanaume anakua ameenda kwa michepuko ila si kweli, akiamua kwenda huko ataenda hata kwa sababu nyingine.
 
Aisee kweli hapa mtaa wapo wa aina hiyo...

Ila nyumba ya pili kuna jamaa tunaendaga nae kwenye mechi na shemeji...Huyo shemeji ni noma mpaka kubet anabet,, aisee wanawake wengine hawataki mchezo..

BTW nadhani ni suala la uaminifu na kuelewana tu.. Kuna wanaokubali, wengine hawakubali!
 
Mimi binafsi nikiri kuwa na mpenzi na shabiki mkubwa wa mpira wa miguu na michezo ya mieleka, kwa wale wanaofatilia mpira wa ulaya kuna mechi za katikati ya wiki huwa zinachezwa usiku sana mara nyingi huanza kama si saa nne na dk 45 basi saa tano kamili usiku.

Nilikuwa lazima niende kwenye mabanda ya video au bar kuangalia kitu ambacho nilijua na kushuhudia kikimkera sana mpenzi wangu japo alikuwa ananiruhusu niende nilikuwa namwona hana furaha nikajionja nikasema huu mpira utakuja kuvunja ndoa yangu.

Nikajichanga changa nikaamua niende kununya DSTV ili niwe naangalia nyumbani mpenz wangu alifurahi mno siku naenda kununua nikakuta kaenda kununu kuku wa kienyeji akasema leo mme wangu ninafuraha sana akatengeneza juice ya embe nikamwona mda wote anafuraha na kukaa karibu yangu.

Nikamwambia kulipia kifurushi kikubwa hicho unaangalia mechi zote ni 184000/= akaniambia we unashilingi ngapi nikamwambia nimebaki na 100000 tu Akaingia ndani akanipa 100000 akaniambia keep change, mke wangu namjua bahili sana siyo kutoa laki haraka haraka ndipo nilipojua nilikuwa namwumiza sana.

Sasa napenda nisaidiwe wanawake mnaumia kwa kiwango gani tunapotoka kwenda kuangalia mpira usiku? Huku mkijua waume zenu ni wanazi wa kutupwa wa mpira.
Lipiaga 122500 utapata zote pia
 
Aisee kweli hapa mtaa wapo wa aina hiyo...

Ila nyumba ya pili kuna jamaa tunaendaga nae kwenye mechi na shemeji...Huyo shemeji ni noma mpaka kubet anabet,, aisee wanawake wengine hawataki mchezo..

BTW nadhani ni suala la uaminifu na kuelewana tu.. Kuna wanaokubali, wengine hawakubali!
shikamoo yangu mpe Shemeji (anabet)
 
unauliza wanaumia kias gan as if yan hakuna faida wanayoipata wengneo....je umejiuliza wanatumiaje muda ambao waume/mabwana wanakuwa wameenda kuchek mpira?
 
Back
Top Bottom