Za jioni wakuu,
Kiukweli nimekuwa katika sintofahamu ya jinsi ya kuwasaidia hawa Dada zetu walio olewa.
Nimekutana na mdada rafiki yangu katika kuongea akanipatia namba ya simu lakini ukimtafuta umpati siku zimeenda akanipigia nikamuuliza vipi akajibu poa mbona haupo hewani akaniambia simu imeharibika hii yenyewe nimeazima. Nikamuuliza sasa umetuma maombi ya kazi wakikupigia si watakukosa kiukweli nilisikitika nikamwambia hata kijisimu cha 15000 si ununue akajibu sina hela ila nikipata nitanunua.
Kilichoniumiza ni kutopatikana kwake halafu pia ameomba kazi sehemu mbalimbali anasubiri kuitwa sasa watampataje na hana simu?.
Nilifikiria nimtumie hela kidogo anunue simu nikawaza ni mke wa mtu nisijeonekana nataka niharibu ndoa za watu.
Swali je ivi inawezekana kumsaidia mke wa mtu katika hali kama hii kwa kumnunulia simu ili akipigiwa na MHR apatikane kirahisi au tuwaache wapambane na hali za waume wao?