apologize
JF-Expert Member
- Jul 22, 2015
- 709
- 568
Habari wakuu,
Hii kitu imenitokea kwangu na ninahisi mwanaume mwezangu simtendei haki, kuna binti mmoja nilikuwa naye kwenye mahusiano kipindi cha nyuma, tukapotezana takribani miaka miwili, kutoka na shughuli za kimasomo na wakawa wamehama mkoa moja kwa moja.
Mimi na yeye tukakubaliana tuvunje mahusiano yetu na tukayavunja kwa amani,miezi kadhaa iliyopita nikapokea sms akinilaumu kwa kukaa kimya sana mimi nikamjibu, simu nilibadilisha hivyo namba nyingi nilikuwa nimezipoteza na hiyo namba aliyonitext ilikuwa ni ya airtel,kwa kuwa mimi sina laini ya airtel nikashindwa kumwangalia kwenye airtel money nijue ni nani? Zaidi ya kumwambia nimepoteza namba nyingi naomba ujitambulishe akasema OK, lakini akagoma kusema yeye ni nani, na mimi nikaamua kupotezea siku hiyo kutokana na majukumu kunibana.
Sasa kuna siku rafiki yake akanipigia simu akaniambia fulani nimekutana nae Dodoma na sasa hivi yupo huko Dar, nikasema naomba namba yake akanitumia sasa kuisave na kumtumia text ya salamu nikaikumbuka hii namba baada ya simu kuonesha text za nyuma naamini hapo mmenielewa smartphone zinavyoonesha chat history.
Baada ya hapo tuliwasiliana na kupanga kuonana, akanielekeza nikamfata mpaka alipo kuwa kwenye duka la nguo la mama ake tukapiga story sana na cha ajabu mapenzi yakaanza upya tena kwa kasi ya ajabu.
Sasa Jana akaniambia niende kwao mambo sikukuuu nikamtembelee nikatimiza wajibu wangu nikafika kutii mwaliko, sasa kuna namba nilikuwa nashida nayo ambayo yeye alikuwa nayo, akaniambia chukua kwenye simu akaniachia simu yake, huwa sina tabia ya kukagua simu ya mtu, Jana uvumilivu ukanishinda nikasema leo ngoja nizame kwenye sms zake.
Nilichokikuta huko ni binti kulalamika jamaa wake kuwa mbona umechelewa kunitumia pesa na jamaa kugomba pesa zote umepeleka wapi nilizokupatia mwisho jamaa akamwambia subiri mshahara wa Mwezi huu ukitoka.
Hili swala nimelileta kwenu mnisaidie kimawazo, maana naamini mawazo ya wengi yananguvu nifanye nini juu ya binti huyu? Kuniomba hela huwa hataki, mimi nikimpa ni kwakulazimisha sana, kitu kingine nilimuuliza kama hatarudi Dodoma akasema harudi kuja huku ndo moja kwa moja,hii inamaanisha ni vigumu kuonana na huyo mpenzi wake aliyepo huko Dodoma.
Hofu yangu sijui mimi wana malengo gani na huyo jamaa wake maana kwenye sms zake nimekutana na mambo mengi waliyopanga na huyo jamaa wake pili kwangu ndo kaniganda balaa hadi aninitambulisha kwa ndugu zake na kuning'ang'ania niende kwao mara kwa mara.
Naombeni ushauri kwa hili na sipendi ajue kama nimekagua simu yake na kukutana na mambo mengine huko.
Nawasilisha