Wanaume wenye hela ni kila kitu japo muda mwingine inawagharimu

Miss Neddy

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,681
8,707
Hi wana MMU

Nimeileta hii kitu tujadili, wanawake siku hizi wanataka mwanaume mwenye hela/uwezo fulani ili wachune na kula ujana wao vizuri (sio wote) ila jicho la tatu je wanaume wenye hela hawa deserve mtu anayewapenda wao kama wao bila kujari hela? au kisa wanahela wakubali kuchunwa? pesa iwafanye watumwa wasi enjoy real love?

Ni ngumu ukiwa na hela mdada kukukataa japo hakupendi atajikaza hivyo hivyo ili afaidi mema ya nnchi na wanawake wanavyojua kuigiza sasa utajiona wewe ndo wewe kakufia kwako hapindui.

Je msalaba huu wa aina yake wenye hela wafanye vipi kupata true love?

TUJADILI
 
Umenikumbusha mbali kweli wala si uongoooo!kuna rafiki yangu mmoja yeye mtaji alio nao ni uzuri tu! mnyamwezi wa Tabora huyooo! Na alikuwa yeye dudu isio na mkwanja akhaaaaa! Akampata mkaka waambiwa mfanyabiahsara wa mazao mkoani! bandidu bandidu! yule kaka alikuwa anamfatilia bi dada, bi dada akawa hajavutiwa kabisaa, maana mnyaki yule sura ya kazi! na wanyakiusa wako strict! watu wakamtia ngumu acha usegeremaa wewe, sura kitu gani, sura inaliwaaa? thubutuuuuuu! Akaambiwa kupenda kaumbiwa mwanaume mwanamke anajifunza kupenda mbele kwa mbele! ajiongeze atafute maisha hela pale ipooooo!

Akakaza nafsi kumzoea yule kaka, kaka akawa anampend yani, anamtoa out, anamzukia jioni, simu nini aaaaaah! mpaka wakazoeana! siku ya kwanza kwenda ku duuu waambiwa wamelala lodge kaja na kibegi kimejaa minoti ya msimbazi kashusha mchele hapo! anafungu begi dada aone mihela vizuri! Akamwambia hapa kiko kiasi kadhaa, ikipungua mia nina wewe! Mechi kali ikapigwaaa! Asubuhi kaesabu mpunga aaaah uko fresh! Bi dada katoa ufundi wote hadi reserve anajua nauli ya maana! Hiiiiiiiiiiiii! Mda wa kuondoa hajapewa hata sh 10 kipande!anaaga mara 10,akaitiwa tax nayo kafanya kulipwa dereva! Mia hii 100kushikishwa hamnaaaa! tobaaaaaa! akajakusema nimefanya kazi ya kanisaa! hio mechi nimetoa sadaka potele poteee simtaki huyu baba!

Hahahaaaaaaa! akaja saluni kwa jimama letu kuleta mrejesho! Akaambiwa punguza pupaaa! Anakupima tu imani! we kaza nafsi mkopeshe mkopeshe hivo hivo siku ya kulipia umkomoe! Dada yetu dada la dada wa saluni hashindwi jambo! Basi akajiongeza mara 3 mechi zote mkopoooo! Hahahaaaaa! Unakula unakunywa na tax anakukodia! Mia senti tano hupati! alioleta mrejeshosaluni tukawa tunapingana mwenzangu, wengine tunasema ajaribu tu kumuomba, wengine apotezeee tu sio riziki hio!

Akiwa hajaamua akatambulishwa kwa dada wa huyo kaka! Yani malengo mazuri tu sema kupewa japo sh 100 hakunaaa! Akamkaribisha na saluni, ukala kuku mwanzo mwisho, dada la dada kapewa 100,000 ya kunywa bia bibie hata sh 10! Thubutuuuu! Dada akasema mi basi nabwaga manyanga!Dada la dada akasema ngoja nizungumze nae! Ndo akamwambia kaka huyu msichana, mpe hela kidogo kujikimu! akajibu mimi nina hleaaaa! naweza kununua malaya yoyote hadi wakiarabu hata wakisomali, ila huyu sio malayaaa, mi nimempendaa, nataka tufaidi mambo kama wapenzi tu sio kudaiana! funguo ya kwangu nimemgea huyu! Kama yeye kakutuma anataka pesa haina shida mie pesa nitampa si nampenda bwanaa ila mahusiano basi! Kampe hii 300,000 namlipa kwa mechi za nyuma! dada la dada ushangingi wote likamshukaaa!Basi ndo akawa akipigiwa huyo kaka hapokei simuu! Akawa anamrushi 300,000 kila mwisho wa mwezi, na simu hapokei wala hamtafuti! Bi dada hela kaiona chungu!Analia tu!

Ilibidi kikao kikali kikalwe wakasuluhishwe! Saiivi wanaishi wote na bi dada kaacha njaa njaa zakeAMETULI TULI KAMA MAJI YA MTUNGI ANAPIGWA FREE P TU! HAHAHAHAAAAAAAAA!
 
Wasipende kumwaga mipesa hovyoo,, kama mwanamke anakupenda anakupenda tuu na sio lazima umpe hela,, mfano utoaji wa hela uwe na sababu za msingi mfano anakuambia anaomba hela ya kununua weaving 400,000 na mwanamme unatoa,,au sijui akanunue CL ya milioni moja..

Au mwingine anaamua kumlipia ada ya chuo mwanamke hata hajamuoa,,hapo unategemea nini?? Kama wazazi wake hawana uwezo wa kumlipia basi subiri ukimuoa ndio umsomeshe.

Mfano unaweza msaidia mwanamke kama kweli kwao wanashida sana na unalitambua hilo lakini kama wazazi wanao uwezo wa kumfanyia shopping,, hakuna haja ya kumpa hela mwanamke wa hivyo.. Unaweza kumpa zawadi ndogondogo ambazo bado zinaonyesha unampenda mfano lotion anayopenda,, deodorant na nk..
 
Hi wana MMU
nimeileta hii kitu tujadili,wanawake siku hizi wanataka mwanaume mwenye hela/uwezo flani ili wachune na kula ujana wao vizuri (sio wote) ila jicho la tatu je wanaume wenye hela hawa deserve mtu anaewapenda wao kama wao bila kujari hela? au kisa wanahela wakubali kuchunwa? pesa iwafanye watumwa wasi enjoy real love?
na 1. ni ngumu ukiwa na hela mdada kukukataa japo hakupendi atajikaza hivyo hivyo ili afaidi mema ya nnchi na 2.wanawake wanavyojua kuigiza sasa utajiona wewe ndo wewe kakufia kwako hapindui lol
je msalaba huu wa aina yake wenye hela wafanye vipi kupata true love? TUJADILI

mi nikushukuru tu kuzikukumbuka hz point 1na 2 sina cha kuongezea!!!!!!!
 
Mtoa mada nae ni mwanamke experince yake ni muhimu

hivi kila anaetoa uzi atoe na experience yake ingekuwaje???? anyway to me money is not my priority, character comes first ingawa free p pia kwangu ni big no
 
hivi kila anaetoa uzi atoe na experience yake ingekuwaje???? anyway to me money is not my priority, character comes first ingawa free p pia kwangu ni big no

Si baridi wala moto wasimamia upande gani?????

free p hutaki... hapo hapo money is not your priority mmmmh..

Haya huyo anaekugonga kwa free P character ikiwa nzuri bado utakua hutaki??????
 
Ulichosema ni kweli kabisa...
Wanatia huruma ingawa kuna wanaowaonea gere na ela zao...

Hata wakipendwa kweli bado wanakuwa na wasiwasi kama ni kweli au influence ya pesa...
Na ndio maana wengi wako very rude...wana midomo michafu kwa wapenzi wao kwani hawana imani nao...

Kuna wengine wanaamua ku mingle na wenye ela wenzao ...

Hii ipo sana Nigeria watoto wa ma bilionea wanaoana wao kwa wao...hawataki gold diggers...
Hata kwa Obama mnaona ma supa staa wanaoana wao kwa wao...gold diggers anawataka nani?
Japo mnaweza sema ubaguzi...
 
Si baridi wala moto wasimamia upande gani????? free p hutaki... hapo hapo money is not your priority mmmmh..

hahaha naona mmeanza kunia attack mdogo mdogo tu focus kwenye mada napenda mwanaume anaeweza kutimiza majukumu yake bhana
 
Ulichosema ni kweli kabisa...
Wanatia huruma ingawa kuna wanaowaonea gere na ela zao...

Hata wakipendwa kweli bado wanakuwa na wasiwasi kama ni kweli au influence ya pesa...
Na ndio maana wengi wako very rude...wana midomo michafu kwa wapenzi wao kwani hawana imani nao...

Kuna wengine wanaamua ku mingle na wenye ela wenzao ...

Hii ipo sana Nigeria watoto wa ma bilionea wanaoana wao kwa wao...hawataki gold diggers...
Hata kwa Obama mnaona ma supa staa wanaoana wao kwa wao...gold diggers anawataka nani?
Japo mnaweza sema ubaguzi...

hata mama yake dangote anatoka datanta family. one of the wealthiest family in africa toka enzi na enzi.

hata mimi ningetoka familia tajiri ningehakikisha naoa binti anayetoja familia ya kitajiri mwenzangu.

ndege wafananao huruka pamoja.

mtu kama dewji akaoa ndala ndefu. au mtoto wa mafuruki amuoe lara 1 au kingasti wapi na wapi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom