Wanaume wapole

Joined
Dec 4, 2014
Posts
9
Reaction score
3
DARASA LA MAPENZI UNAJUA NI KWANINI WANAWAKE WENGI HUPENDA WANAUME WAPOLE...?? SOMA HAPA NIKUJUZE.

Ukimuuliza binti yeyote mwenye ndoto ya kuolewa,,akutajie sifa za mume ampendae,sifa ya "awe mpole" itakuwa ktk orodha ya mwanzo kabisa.Katika utafiti binafsi sifa hii imetajwa na wasichana 74 ikiwa ya kwanza,,wasichana 113 ikiwa ya 2.

Lakini kwa wanawake walio ktk ndoa,,wanawake 20 walisema wanapenda mume mpole ikiwa sifa ya 1 na 42 waliobaki waliitaja ikiwa ya 2 Huo ni utafiti binafsi ambao ulitaka kujua tu UPOLE WA MWANAUME una nafasi gani kwa mwanamke Lakini kwa nini wanawake au mabinti hupenda mwanaume mpole? Kwa nini mkorofi hatajwi kabisa?

Je ni kweli ni watu wanaohitaji huruma kiasi hicho? Mtaalamu wa masuala wa mahusiano wa kimarekani Baruck Miller aliyetafiti mahusiano kwa miaka zaidi ya 20,,anasema "... Mwanamke anampenda mwanaume mpole ili AJITAWALE KTK MAHUSIANO..." Siku zote,mwanamke anapenda awe huru kwenda apendapo au kupewa atakacho. Hivyo anapokuwa mbele ya mwanaume mpole hana wasi,,wala hana tabu ya kutimiziwa shida yake.

Akikutana na mwanaume mpole sana kiasi cha kukaribia ujinga basi atamuendesha mume/mpenzi kama rimoti control.

Jambo wanalosahau wanawake ni kuwa,,upole wa wanaume wengi wanautafsiri kama ujinga,uzezeta au kuliona kundi hili la kuchuna wapendavyo.

Laiti wangekumbuka kuwa mwanaume mpole ni kama volcano tuli ikilipuka imelipuka basi sifa ya upole ingekuwa ya mwisho.
 
Duh mimi ni mpole sana, karibuni sana kwangu. Hahaahhahhahaaaaa wanawake wanaogopa kipondo ili wawapande vichwani waume zao
 
Duh mimi ni mpole sana, karibuni sana kwangu. Hahaahhahhahaaaaa wanawake wanaogopa kipondo ili wawapande vichwani waume zao

Sasa we uko tayari kupandwa kichwani watu wachangamkie fursa?!
 
Nikweli wanawake wanapenda wanaume wapole ila siamini kua sababu yao ni hiyo ulioitaja.

Mtu mpole mara nyingi ni msikivu/muelewa. Hiyo inaweza kua sababu maana wanawake wanapenda kusikilizwa japo usitoe solution ya hicho ulichosikiliza.......
 
Nikweli wanawake wanapenda wanaume wapole ila siamini kua sababu yao ni hiyo ulioitaja.

Mtu mpole mara nyingi ni msikivu/muelewa. Hiyo inaweza kua sababu maana wanawake wanapenda kusikilizwa japo usitoe solution ya hicho ulichosikiliza.......

Kuna kaukwel ndani yake
 
Anhaaa ndio maana yule dada akaniuliza "hivi wewe kaka ni mlokole?"
 
Huyo mtafiti alisahau kuainisha kuwa huo upole unasababisha pia wengi waliwe kirahisi...!!!
 
Na wanakazwa na kuachwa iman hii potofu....
Naenjoy kuonekana mpole
 
Upole my ass.
Kila chenye sura hakikosi kisogo.
Atakuwa mpole Hana mbinu za kudaka mkwanja. Mtakula huo upole wenu hadi mvimbiwe
 
Inabidi tufasiri kwanza maana ya mpole. Binafsi naona mtu mpole is boring. I love a man who is talkative, charming, aggressive, hits things head on, has a million ideas and can enjoy anything. Naamini kinyume cha upole sio kuwa abusive. Mtu anaejiamini kamwe hafikirii kuwa kapandwa kichwani
 
Ivi niulize mpole anakuwaje? Manake huyu Wangu akikasirika anapenda kunambia ivi unanichukuliaje? Unanichukulia poa eeh? Kucheka nataka nabaki namtizama tuuu, lakini siku hiyo ujue kufanya kazi Za ndani kutanikhusu...
 
mwanaume mwenye kuongea ongea sana km mc mi simpendiii
 
mwanaume mwenye kuongea ongea sana km mc mi simpendiii

kuongea sana siyo tatizo....tatizo hicho akiongeacho kama ni pumba ama kinajenga......

sababu kuna mtu anaongea maongezi ambayo hakuboi bali utapenda kumsikiliza muda wote........siyo unatoka na mtu usipoanzisha wewe story basi mnakuwa kama mabubu.....nah my dia napenda muongeaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…