Wanaume waliochelewa kuoa wana msongo wa mawazo kuliko wanawake

Status
Not open for further replies.

agata edward

JF-Expert Member
Nov 25, 2014
6,641
9,400
Kuna utafiti nilikuwa nafanya baada ya kufwatilia baada ya kuona topic nyingi zinazowasema single mother's na wanawake waliofika miaka 30s bila kuolewa.

Nilichokigundua;

1. Wanawake waliochelewa kuolewa na na single mother wengi wana amani ya moyo kuliko wanaume waliochelewa kuowa na single dads ndomana awaishi kujaza JF topic za kuwazungumzia wanawake hiyo yote nikujipa moyo ili kupunguza maumivu.

2. Wanaume wengi waliochelewa kuoa mpaka kufika miaka 35 na kuendelea wengi walitegemea kuchelewa kuoa kutawafanya wawe na pesa na maisha mazuri lakini imekuwa tofauti wengi wamefika umri huo wakiwa hawana kitu tofauti na wenzao waliooa mapema wana faraja ambayo ni watoto na wengine wamepata baraka maisha yamewanyookea,asila za kukosa vyote vinawatesa wanajikuta na asila muda wrote poleni kwa hilo.

3. Wanaume wengi waliochelewa kuoa wanatabia zisizovumilika bila kusahau maneno mengi bila vitendo ujuaji mwingi na dharau kwa wanawake wanasahau walizaliwa na mwanamke poleni, mwanamke yoyote anatakiwa kuheshimiwa.

NB; Jirekebisheni tabia njema si kwa mwanamke mtu hata mwanaume unatakiwa ujitambue labda ujitahidi uwe na mapesa kama Mengi ndo utapata mtoto mzuri wakutuliza moyo wako ukifika 40s maana huwa mnajipa moyo wanaume amzeeki.
 
Pole sana single mother wewe

Acha kuwafuatilia wanaume, jikite zaidi kumcare huyo mwanao

Kwa taarifa tu, mwanaume ataikaa hadi zaidi ya miaka 45 yeye maisha safi tu na ataendelea kuongeza idadi ya single mum bila stress
 
Naona ushaanza kuwasema watu kisirisiri...........................
 
Pole sana single mother wewe

Acha kuwafuatilia wanaume, jikite zaidi kumcare huyo mwanao

Kwa taarifa tu, mwanaume ataikaa hadi zaidi ya miaka 45 yeye maisha safi tu na ataendelea kuongeza idadi ya single mum bila stress

Hahaaaa nimeona kajipa moyo eti single dads. Duuuuh Tanzania hii kuna single dads kweli na utitiri wa wanawake wa kutusaidia kulea?? Labda useme kina sie wagane
 
Hahaaaa nimeona kajipa moyo eti single dads. Duuuuh Tanzania hii kuna single dads kweli na utitiri wa wanawake wa kutusaidia kulea?? Labda useme kina sie wagane
Ahahaha
Mkuu sijawahi sikia hii kitu et single dad
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Usilazimishe mawazo yako yaaminike kwa kusingzia kigezo cha tafiti hewa

mwanaume hawez kuwazia ndoa mpka apate msongo ili hali akitaka papuchi mnampa pasipo ndoa awaze ndoa yann???

Ukiona mwamke ana aman ya moyo na ndoa hana ujue amesha gv up juu ya ishu nzma ya kuolewa amejilazmisha kukubali uhalisia na ameweza kuwa confortable kuendelea na maisha yake
 
huo ni ukweli kabisa! mwanaume unafikaje miaka 35 hujaoa wakati wanawake ni wengi mara tatu ya wanaume .bora sisi wanawake inajulikana wanaume ni wachache! napenda mwanaume wa miaka 40 ila najua ni kimeo tu na bomu acha linilipukie tu .
 
Inategemea unalitizama jambo hilo kwenye kona ipi.
Kwa mfano: Kuna watu wanaamini kwamba maisha yao hayawezi kukamilika bila kuoa. Watu wa namna hiyo wakichelewa kuoa, kweli wanaweza kujikuta kwenye msongo wa mawazo.

Lakini pia, kuna wale wanaoamini kwamba maisha yao yamekamilika, na yatakwenda, bila kujali wameoa au hawajaoa. Watu wa namna hii, hata ikitokea wamechelewa kuoa, hawawezi kupata msongo wa mawazo unaouzungumzia.

Labda niongeze kitu hapo: Msongo wa mawazo au depression, ni tatizo la kifikra zaidi. Ni tatizo lisiloangalia kama umeoa au hujaoa. Vile unavyowaza ndivyo utakavyokuwa. Vile unavyoamini ndivyo itakavyotokea. Kwa hiyo inategemea hao unaowazungumzia, fikra zao na imani zao wameziweka upande gani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom