Wanaume wa Pwani

Naomba wadada wenzangu mnijuze, ni kweli kwamba wanaume wanaotoka makabila ya ukanda wa pwani kwa maana ya mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Tanga, Lindi na Mtwara wanaweza mapenzi kuliko wanaume wanaotoka mikoa ya Bara?
Nawasilisha
 
Una maana gani unapoandika "wanaweza mapenzi" ?

Tungo tata hiyo.
 
Ah kumbe hii ni kwa ajili ya wadada, mkuje huku mumweleweshe mwenzenu, anataka kuzijaribu.
 
ninamaanisha wanaweza kunako 6 kwa 6, na ujumla wake
 
mmmhhh...!!!sio wote sasa hivi wanaume bwana huwezi kumhukumu kwa kabila lake kiukweli kabisa maisha yamebadilika sana maana mi nna asili ya pwani ila nimeolewa bara
hapa nilipo kuna watu kadhaa hawawataki wabara hata kuwaskia na nikiwa pwani
wa pwani hawataki wa wenzao pia kwa vigezo mbalimbali
sasa hivi inategemea mtu na mtu
 
Ukabila ushaisha siku hizi mtu anaweza kuwa wa Pwani lakini akawa nanga kuliko wa bara huo ni ubunifu wa mtu binafsi haijalishi anatoka wapi.
 
Asante mpendwa
 
Sio kweli kabisaaaaa, kwanza nikulize kujua mapenzi Kwa fikra zako wewe ni vp? Unadhani kukata mauno ndio mapenzi? Au kuchelewa kuuuu?? Ndio mapenzi? Mapenzi ni fani ya mtu anavyo kujali kukuthamini, kukuheshumu na ku kupenda Kwa dhati hayo machezo hata Kama ujui utafanyaaa Mpaka utajiuliza Mimi huyu au mwengine? Kwa hiyo Sio wa pwani tuu hata wa bara hodari mashallah....
 

Umenigusa ndipo shostito, mumewangu mbara na ananipagawishaaaje!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…