Wanaume TUSINYANYASE wanawake..!

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
1,487
Reaction score
914
Sijui niseme ni Kasumba, au Tabia, au upofu labda ndio mfumodume wanaoungea walimwengu ingawa siujui Vema Kwa hii Tabia Yetu wanaume..

Inaonyesha Wanaume hatuna control wala vidhabitimwendo pale tunaposikia wake/wapenzi wanatusaliti..

Inaanza Sasa kuzoeleka Ndani ya Jamii Zetu matukio ya kuuana Kwa risasi kisa kikiwa wivu wa Mapenzi. Wanaume wakifumaniwa Na wakati mwingine fumanizi linakuwa live Na wakati Mwingine Ndani ya Nyumba/chumba chao lianaume linafumaniwa likivunjavunja amri ya ngapi sijui kwenye Vitabu vya Haki.. Lakini Mbali Na michakatojoto yote misamaha inatembea Na maisha yanasonga Mbele , kinamama wanasemahe sana hawa ..

Itokee Sasa Mwanaume afumanie, HASIRA zake hazidhibitiki, nyakati Za nyuma kabla ya Mzinga au Tanganyika Arm au Hawa wengine hawajaanza kutuuzia Silaha, Na Sheria ya raia kumiliki silaha haijaingia Kwenye jamvi la nchi yetu , mwanaume akifumania Kama mkono Wa Kufa Mtu hautachezwa Basi mapanga, marungu, visu n.k vilikuwa vikitumika. Faida Za matumizi ya zana hizi za kale ni kupata majeruhi Na ikitokea tukio la kifo Basi sanasana ni Mtu mmoja wakizidi sana wawili. Lakini kizazi Cha Leo, ambapo Mwenye Pesa Ndani ya wiki mbili unanunua na kukamilisha taratibu Za kumiliki silaha.. Ni hatari zaidi. Akifumamia haui mmoja tu analenga shabaha yake as if yuko Kwenye movie Na kunyofoa ROHO Za wengi within a single shot.. PAH..!!.

Labda hii Sheria iangaliwe upya, Silaha tunazomiliki wengi hatuzitumii kujikinga Bali kulipa vizasi. Matukio mangapi ya Ujambazi mitaani wala hatusikii mwizi kanyukwa kitu Na jirani. Wevi wakiingia watu ndio kwanza tunaficha vibastola mbaliii ili mwizi asikione Na kukikwibwa badala ya kukitumia.

Kuna mamia ya mashtaka Kwenye karibia kila kituo Cha polisi Na mengi yanamalizwa hapo hapo Na mengine yanavuka Kwenda mahakamani ya kutishiana Silaha Kwa wanandoa, marafiki au kwenye sherehe Na asilimia kubwa ni Mambo ya Centre of Gravity (Mapenzi). Na Wanaume ndio hasa VINARA Wa kuvichomoa Na kutaka kuonyeshea kaufundi flan.

Nadhani Wanaume tuachane Na manyanyaso haya. Kama silaha si Kwa ajili ya self-defense irudishwe. Kuna kisa kimoja hapa nikusimulie..

Siku moja nilimpick jirani yangu Wa Nyumba ya tano hivi nadhani siku hiyo hakuwa on. Labda aliamua. Tukiwa wawili Baada ya kitambo Cha story Za pale Na huko hasa Ulinzi shirikishi mtaani kwetu nikamdokezea Kwamba naskia Mara Kwa Mara huwa ana Ugomvi Na Mke wake, anyway hayo ni mambo Binafsi utajua how to solve kila familia Ina mapungufu yake ila my concern Ugomvi ukiwa Kwenye Chorus huwa nasikia unakiibua kimguu Cha kuku Na kutishia tishia hivi.. Jamaa kabla sijamaliza akanidakia .. " unajua bro, wanawake watu wa ajabu sana, wakorofi kweli, sometime lazima umtisheflan ili Adabu iwepo. " nikamwambia kwanza hilo ni kosa kisheria lakini pia hasira hazina macho iko siku kikombe kitajaa Na utaandika historia.. " tukapiga story safari ikasonga ..

Baada ya wiki Tatu, jirani Yake nyumba ya pili, alivamiwa na sijui vibaka au wevi wa usiku, majambazi hawaibi usiku. katika harakati Za kuvunja geti Yeye akawa anachungulia mchezo wote dirishani akiwa chumbani kwake akitetemeka, Naskia mkewe akamwambia achukue bastola Yake afyatue juu.. aliposikia anaambiwa achukue bastola jamaa alivunja dirisha lake la kioo Na kufyatukia nje mbio akatokomea Kwenye kichaka nje ya Nyumba Yake, mkewe kuona vile akakurupuka akapindua sehemu silaha ilipo akaichukua Na kuitupia nje vichakani alikotokomea mume wake. Kisha kukawa Na ukimya Kwa muda. Kumbe Zile harakati Za mwanaume kuvunja dirisha Na makelele ya kishindo akitimka viliwastua majambazi Nao wakaahirisha zoezi Lao Na kutimka.

Baada ya Nusu saa majirani wamekusanyika( sikuwepo nilikuwa safari) Yule jamaa akaibukia mafichoni..wakamuuliza kwanini alisepa akasema mkewe alipomgusia juu ya bastola akaona wakiingia huku ndio wataanza Na Yeye akaogopa Na kukimbia. Mkewe Naye akaona wakiingia wakakuta silaha patakuwa padogo bora aitupilie nje huko.. Silaha ikatafutwa Na kupatikana.. Kama kawa Baada ya masaa mawili ndio polisi wanafika.. Chezea wezi.. !!
 
Ni kweli mkuu maana wanaume wengi ni wanyanyasaji wa mama na dada zetu!
 
Ila sometimes warembo wanatunyanyasa pia, tusielemee upande mmoja
 
Hata wao wanatunyanyasa ila hawatumii nguvu nyingi kama sisi kulipa visasi! Shame on us! Tunawatendea mangapi machafu na wanatusamehe??
Kwanini sisi si wavumilivu na tunashindwa kupima adhabu tunazotoa?
We need to change! Ubabe huu tuuelekeze kwenye kutafuta fedha for the well being of our families.
Kutumia maguvu mengi pasipo akili ni ujinga na hasara!
Naunga hoja mleta mada
 
Kuna wamama jana kwenye daladala niliwaskia wamesema nao wanakuja na njia ya kujibu mashambulizi, Sasa sijui itakuaje manaake kila mmoja anmuwinda mwengine
 
naunga mkono hoja..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…