ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 46,758
- 100,788
Nimekuwa nikitafakari sana juu ya malezi watoto wetu. Ni dhahiri kuwa kulea mtoto peke yako ni changamoto sana, kuanzia kutafuta mahitaji ya kila siku ya mtoto hadi kumtimizia mahitaji yale kuanzia asubuhi hadi usiku. Hii kazi inahitaji wazazi wote wawe bega kwa bega ili mtoto afurahie na wazazi wafurahie zawadi hii toka kwa Mungu.
Swali fikirishi kwa wenzangu wanaume, tumekuwa na kasumba ya kuzaa "ovyo", bila kujali mustakabali wa watoto wetu, bila kujali tutawalea vipi, tutawaandaaje kupata elimu bora ya kidunia na ya akhera(mbingu).
Lakini pia tumekuwa wa kwanza kuwanyooshea vidole hao wanawake tunaowazalisha, hawafai, hawana jema, ni malaya n.k.
»Kweli kama mwanaume unajisikiaje kuzaa watoto nje, possibly na wanawake watatu-wanne tofauti?
»Unajisikia vipi kuishi mbali na watoto wako?
»Ukiona watoto wa mitaani, hukumbuki kuwa kuna watoto wako umewatelekeza na huenda nao wakaishia kuwa ombaomba?
»Kwa nini hutaki kuwa sehemu ya malezi ya watoto wako, ili wakiwa watu wazima nawe ujivunie kazi ya mikono yako?
»Hivi mnasahau kuwa yule mtoto uliyemuacha huko ndiyo "identity" yako, kwa nini usifanye jitihada za kumlea? Hata kama kwa bahati mbaya huwezi kuishi na mama yake, basi hata kumlea?
Kuna uzi mmoja watu walifunguka sana kuhusu utoto wao, wengi walikuwa wanalaani kutelekezwa na wazazi wao hasa baba. Ni wakati sasa tubadilike, tulee watoto wetu katika misingi bora ili waje kuwa watu bora kwenye jamii zetu.