Tape measure
JF-Expert Member
- Nov 26, 2015
- 1,980
- 3,578
Naandika huu uzi kwa hisia Ni mkasa uliomtokea huyu Dada wiki Jana.
Ilikua ni siku ya jumatano akamwomba Boss wake ruhusa ya siku mbili yaani Alhamisi na Ijumaa. Lengo ni kwenda jiji la mwendo kasi kuonana na mchumba wake ambaye alihamishwa kikazi kutoka Iringa kwenda jijin Daslam.
Alhamisi asubuhi msichana akapanda basi kutokea Iringa -Daslam. Ikumbukwe ndio mara yake ya kwanza kwenda kumsabah mchumba wake tokea ahamishiwe jijin Daslam. Mawasiliano yakawa ya kusuasua kwani mchumba wake alidai yuko busy iyo siku. Ilipofika majira ya sa 7:30 msichana akawa anaingia maeneo ya Mbezi mwisho hivyo akaona ni vema amtaarifu mchumba wake kuwa anakaribia kusudi ampokee Ubungo bus terminal.
Mwanaume hakupokea simu Bali akamwandikia message kuwa bado yupo kazini, Dada wa watu akawa mpole na kusonga mbele kimara hatimaye gari ikafika Ubungo. Alfurahi sana kufika katika jiji la mwendo kasi akiwa na mawazo ya kutembezwa maeneo kadha wa kadha na mchumba wake.
Basi Dada wa watu akajisogeza kando na kumpigia mchumba wake simu kuwa tayari ameshuka Ubungo bus terminal. Ilikuwa ni majira ya sa 3 kasoro Usiku.
Maajabu mchumba wake akamjibu kuwa bado yupo kazini na hawataweza kuonana kwa siku hiyo ikumbukwe kuwa huyo mwanaume kazi yake ni accountant wala so mlinzi.
Msichana wa watu akaishiwa nguvu na kuhisi mwili mzima una vibration kwani alijihisi yupo ndotoni. Aliendelea kumpigia simu na kujibiwa kwa message kuwa yupo busy.
Mjini shule, Dada wa watu akabaki ana simanzi takriban dakika 10 bila kujua afanye nini.
Ndipo alipopata wazo na kumtafuta rafiki yake wa siku nyingi na kumuelezea yaliomsibu. Bahati nzuri rafiki yake alikua anaishi maeneo ya Mabibo mwisho hivyo alimuagiza apande bodaboda itamfikisha. Mungu ni mwema akakutana na rafiki yake uyo wa kike wakaelekea katika chumba chake alichopanga maeneo jirani.
Kukakucha ikawa Ijumaa mchumba wake akamtext Sory najua nimekukwanza baada ya muda akamtext tena " Are you still mad at me" msichana wa watu akamjibu Ndio.
Ikawa jumamosi jamaa ake bado anasema yupo busy ikawa Juma pili msichana wa watu ikambidi apande buss kurudi iringa asijepoteza kibarua chake na ndio ikawa mwisho wa yeye na mchumba wake waliedumu tokea mwaka 2013.
Inauma sana japo hatufahamu kwa nini uyu mwanaume aliamua kumfanyia ukatili kama huo ila ni dhahiri mwanamke alikua kamkabidhi moyo wake ndio maana kasafiri Iringa-Jiji la mwendo kasi.
Wanaume tupunguze uswahili kwenye maswala ya uhai wa wanawake. Najiuliza tu angelikua hana rafiki wala pesa ya ziada nin kingempata??
Mateso ya kisaikologia alopata yataweza kumfanya awe katili?
Kwa nini umuadhibu mtu kwa makosa alofanya zamani?
Je hakuwa na njia ingine ya kumwadhi kama alimkosea? Kwanini alimwambia aje Daslam?
Sheria inasemaje kuhusu ukatili kama huu?
Ni hayo tu Wakuu.