Wanaume mwogopeni Mungu

Wanaume mwogopeni Mungu

Fatmata

Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
66
Reaction score
34
Kwa anachonitenda mume wangu nachelea kusema wazi kuwa ni vigumu sana kwa wanaume kuurithi ufalme wa mbingu,tumetoka nae mbali,leo ameamua kunifanyia hivi,jamani naomba ushauri wenu kabla sijafanya jambo baya!
 
Bibie! unadhani bila wewe kueleza amekufanya nini sisi tutajuaje? Huenda hata ww umemkosea mwenzio, hivyo funguka kwanza.
 
Kwa huyo mume wako ndo itakuwa ngumu kuurithi ufalme wa Mungu siyo wote,kwa huyo mwanaume wako mwenye laana ya kutembea na dada yake mpeleke akapigwe maombi uone kama hajakutangulia kuuona huo ufalme wa mungu,Unamjua vema mumeo na nina imani unampenda na nina uhakika hata ww hauamini kama ni akili yake ya kawaida ndo inamfanya akufanyie hivyo.....basi muombee kwa Mungu ambadilishe no way out waswahili wanasema kukimbia tatzo siyo suluhu
 
Fanya moja kati ya hii
 

Attachments

  • 1389360287956.jpg
    1389360287956.jpg
    26.4 KB · Views: 119
Kwa kuzingatia ile post yako ya mwanzo juu ya kusalitiwa na mumeo kwa sababu ya hela, na kwa kuzingatia hali ulio nayo kifikra na kiroho kwa sasa... Ni vigumu sana kweli wanaume kwenda mbinguni. Mwenye ufahamu na afahamu.

Nakuombea upate ufumbuzi wa kudumu. Mungu akuepushie mbali na fikra za kisasi na fikra za umauti (kujidhuru au kurudhu) Mungu akutie nguvu uinuke ujikung'ute usonge mbele. Yeye ndio mlipaji wa vyote na fahamu kama ukiruhusu hekima yake ikuongoze jasho lako halitakuwa limepote bure. Ila ukijichukulia hatua kulipa kisasi unamnyima nafasi ya kukufariji na kukuinua.

Pole sana.

Kwa anachonitenda mume wangu nachelea kusema wazi kuwa ni vigumu sana kwa wanaume kuurithi ufalme wa mbingu,tumetoka nae mbali,leo ameamua kunifanyia hivi,jamani naomba ushauri wenu kabla sijafanya jambo baya!
 
Back
Top Bottom