figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Wananchi wa kijiji cha Saza wilayani Chunya wameamua kufunga ofisi ya Mwenyekiti wa kijiji hicho kwa kujenga matofali mlangoni ili kumzuia mwenyekiti wao kuingia ofisini kwa madai kuwa ameshindwa kuwasomea mapato na matumizi ya fedha za kijiji huku pia wakimtuhumu kuwa ameuza rasilimali za kijiji hicho bila kushirikisha wananchi.
huu ni mwonekano wa mlango wa kuingia katika ofisi ya mwenyekiti wa kijiji cha Saza ambao wananchi wameamua kuufunga kwa kutumia matofali ya kuchoma na saruji wakipinga Mwenyekiti huyo kuendelea kuwa madarakani.
Akizungumza na ITV afisa mtendaji wa kata ya Saza Julius Simwita amezitaja tuhuma ambazo zinatolewa na wananchi dhidi ya mwenyekiti wao ambazo ndizo zimesababisha wachukue uamuzi wa kufunga ofisi hiyo.
Mgogoro huo ukamlazimu mkuu wa wilaya ya chunya Elias Tarimo kufika katika kijiji cha Saza na baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao ikambidi amshauri mwenyekiti wa kijiji hicho kujiuzulu na kuitaka halmashauri ya serikali ya kijiji kuteua mjumbe mmojawapo atakayekaimu nafasi hiyo mpaka uchaguzi utakapoitishwa.
Chanzo: ITV