‘Wananchi ndio wataamua ya Kigamboni’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘Wananchi ndio wataamua ya Kigamboni’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 24, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  NA THOBIAS MWANAKATWE

  24th July 2012

  Wakati serikali ikiwa imekwishatenga Sh. trilioni 11.6 kwa ajili ya ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es salaam, Diwani wa Kata ya Vijiweni, Suleiman Mathew, amesema utekelezaji wa mradi huo utategemea maamuzi yatakayotolewa na wananchi.

  Diwani huyo alitoa ufafanuzi huo juzi (Jumapili) wakati wa akingumza na wananchi wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shimo la mchanga kwamfaayeka.

  Mathew alisema wananchi wa kata hiyo wasiwe na wasiwasi kwani utekelezaji wa ujenzi utategemea wananchi na kuna kamati ilishaundwa na inaendelea kufanya kazi.

  "Jamani sasa mimi kwenda bungeni na kurudi lisiwe tatizo hapana, Dodoma nitaendelea kwenda kadri inavyowezekana na Mtanzania yeyote ana uhuru wa kwenda kuhudhuria vikao vya Bunge, matatizo madogo yaliyopita kati yangu mimi na mbunge tutayamaliza," alisema Mathew.

  Alisema hakuna sababu kwa suala la ujenzi wa mji mpya wa kigamboni kuwa ajenda ya kisiasa na kwamba wanaotaka kujipatia umaarufu kupitia suala hilo wangoje 2015.

  Mathew alisema yeye na madiwani wenzake wataendelea kushirikiana na Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile na kwamba hata juzi amewaaga wakati anakwenda Ulaya kikazi.

  Katika mkutano huo diwani huyo alikabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni tatu, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizotoa mwaka 2010.

  Vifaa alivyokabidhi ni pamoja na kompyuta nne, tenki la maji la lita 4000, turubai na nyenzo za kilimo.

  Akiwasilisha bajeti ya 2012/2013, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, alisema wizara yake imetenga Sh. trioni 11.6 ambazo zitakuwa zinatolewa kwa awamu.

  Wakati wa kikao hicho cha bunge, Mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk. Ndugulile, alisema mradi wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni ni batili kwani umekiuka sheria na kwamba, kinachofanywa na serikali ni kung'ang'ania udalali kwa kutaka kuchukua ardhi ya wananchi maskini na kuiuza kwa bei kubwa kwa matajiri, kinyume cha ahadi yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania.
  CHANZO: NIPASHE


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Madiwani hawa ni Hatari... ni Wapi hao waliopewa PESA na Waziri?
   
 3. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nchi iliisha uzwa, mtake, msitake, mtaondoka!!!!
   
 4. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,927
  Likes Received: 950
  Trophy Points: 280
  Walaji ni walaji tu
   
Loading...