Wananchi Mtwara Mjini wafanya maandamano makubwa kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!

Keep it up Mtwara people!! Yaani nchi haitawaliki tena!! Tuitishe uchaguzi wa urais wa dharura
 
Naomba na ajitokeze mtu na aeleze faida ya Gesi ya Mtwara kubaki Mtwara...

Pia aeleze hasara za gesi ile kupelekwa katika miji mingine kama Darisalama....Kwa watu wa Darisalama, kwa watu wa Mtwara na Kwa Watanzania wote....

Kwa mawazo yangu ya 'kizamani'nilifikiri Mtwara wangepigania kunufaika na maliasili yao siyo kutoisafirisha! Je tutakapogundua mafuta pia tutadai yasisafirishwe kutoka sehemu yalipogundulika kwenda kwa mlaji- this is myopic thinking.
 



hatujapinga hilo

sasa kwanini isafirishwe gesi ghafi??

Ndivo wanavofanyaga huko rusia unakoishi??mana wabongo kwa ulimbukeni hatujambo atii,,
urusi na mtwara wapi na wapi??

Hata mkilia viboko badooo,,,gesi kwanza,mtwra kwanza,tanzania kwanza

siasa baadae
 


Hii siyo tanzania tena, kama hili nalo tunaliona kama ni sawa. Hivi kweli gesi izalishwe hapo na itumike hapo hapo? kweli? hatuangalii hata mifano toka kwa nchi zilzoendelea? siasa gani hizi za kudumaza vichwa vya watanzania na kuanza kuona maandamano kama staili ya kutafuta haki?
 

Kazi unayo leo, naona unahaha kila kona kujaribu kudanganya watu lakini bahati nzuri wananchi wa mtwara wamekwishasema kwa sauti moja, mtwara kwanza vyama baadae.
 
waliibeza sera ya majimbo kwa kuichagua ccm,haswaa kusini

mapato yatokanayo na mlima kilimanjaro hayanufaishi kilimanjaro,TANAPA haina jibu bali serikali ya ccm
 

Mkuu Nabwada, mafilili anatetea kitumbua chake, hawezi kukubali mabadiliko yatakayowanufaisha walio wengi kwa kuwa mfumo uliopo unawaneemesha wao. Wanatetea matumbo yao hawa.
 
Ncha Kaliii....hiyooo.... na kitu kizito kuweni makini, Capitalist(Tz Govt) ni mtu hatari muwe wavumilivu mwisho wake ni ushindi.
 

Wananikumbusha jamaa wa MEND, Ken Saro Wiwa na Ogoniland. Mungu awabariki
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

Hiyo serikali gani inasubiri kuambiwa ndipo iwe sikivu badala ya kutatua kero za wananchi?
Ingawa hawana hoja ya kuandamana kudai gesi isipelekwe Dar, Sikubaliani hata kidogo kuwa maandamano si njia nzuri ya kudai haki. Unataka wachukue mikuki na mapanga? Naona gamba limekushika mpakapuani na kichwa chote huna sehemu ya kupumua mawazo huru.
 
maandamano ni haki yao kikatiba na katiba sio mali ya chadema bali ni ya watanzania wote.
hao wawakilishi unaosema ndo kina hawa ghasia ambao wamewafanya wana mtwara kuwa misukule wa ccm.
ccm imewanyanyasa watu wa mtwara na sasa wamechoka.

Watanzania wameshaona madhara ya kuachia hovyo rasilimali za Nchi ziende kwa watu wachache,upole wa watanzania ndio umepelekea watu wachache kuficha mabilioni Uswis huku wengine wakisema hivyo ni vijisent tu.Wana-mtwara wakomae mpaka kieleweke!...
 

Nabwada achana na huyo ''ashindikene'' anataftia watu ban huyo.
 
Mtwara KOMAENI tu. Hiki kiwanda cha kusafisha GAS na kufua umeme kikijengwa Mtwara, mtapata wafanyakazi wengi sana watakaokuja kuishi huko. Kwa kuwa wengine kipato chao kitakuwa kikubwa, basi wataanza kupeleka watoto wao shule, kufanya shopping, kujenga nk.

Na nyie hata kama hamna shule, basi mtapata kazi za ulinzi, kupanda mauwa kiwandani na kwenye majumba yao, kufagia na kila aina ya usafi. Watataka huduma bora za afya, elimu, usafiri nk.

Kwa ufupi ni kuwa mzunguko wa hela utakuwa mkubwa sana kwenye kiwanda cha Gas na ikiwezekana mitambo ya kuzalisha umeme viwepo pia hapohapo Mtwara. Dar ije Gas iliyo tayari kutumika moja kwa moja.

KOMAENI WATANI ZANGU HADI KIELEWEKE. Nyie ndiyo mmeweka msingi mpya wa kulinda rasilimali zetu.
 

Wasipokaa vizuri wanaweza kuondoka hata kabla ya 2015......
 
..... Haijaniingia akilini... wanaandamana kuzuia gas isije Dar? inaamaana ikija Dar itaisha wao watakosa au? Hapo najiuliza iwapo kila mkoa utaamua kuzuia mali zilizoko katika maeneo yao ingekuwaje katika Tz? .....
 
Hivi maandamano hayo yana uhusiano gani na itikadi za vyama? inawezekana kuna watu wanaandamana hawaelewi kwa nini wanaandamana. Sidhani kama madai ya watu wa Niger Delta yanaweza kufananishwa na hiki kinachoendelea huku Mtwara.
Ni haki yao kikatiba kutoa mawazo yao hatahivyo hawapaswi kupongezwa kwa kufuata sera za kikanda badala ya kinchi
Wanataka kuwe na kiwanda cha kusafisha gesi na kuweka kwenye mitungi ya gesi huko huko Mtwara, ili wapate ajira.

Wanataka pia kuwe na fund maalum inayobaki kwa maendeleo ya Mtwara kwa kila fedha inayopatikana kutokana na gesi hiyo.

Ni madai ya msingi sana, kwani wameachwa nyuma sana, wameiunga mkono CCM sana lakini hakuna shukrani.
 
Nabwada achana na huyo ''ashindikene'' anataftia watu ban huyo.

MMAHE na NABWADA msisahau mlikotoka, serikali ya CCM ndiyo imesaidia Mtwara yenu kufunguka, hadi siku hizi mnapanda mabasi mazuri na kufika Mtwara kutoka DSM saa 7 mchana tofauti na enzi za Akida Bus. Kaeni chini mfuate Mstahiki Meya, Shilingi na Mbunge Murji; mtakuja fanikiwa mkifuata njia ya majadiliano kupitia wawakilishi wenu. CCM ni wasikivu, Sinani ni mtu makini tena anaweka kipau mbele kwa manufaa ya Mtwara. Mkuu wenu wa Mkoa, Kamanda Simbakalia ni msikivu sana, mtumieni ipasavyo kupitia wazee wenye busara kama vile Abdalah Maulidi na Shaibu Bashir
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…